Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiweka jiwe la msingi kuashiraia ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Iringa sehemu ya kutoka Dodoma - Fufu (Km70.9) huku akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa upande wa Tanzania Bi. Tonia Kandiero kushoto pamoja na Mwakilishi kutoka Serikali ya Japan na JICA, Ndugu Kuniaki Amatsu kulia huku Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akishuhudia tukio hilo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Iringa sehemu ya kutoka Dodoma - Fufu (Km 70.9) iliyojengwa kwa kiwango cha Lami. Wengine walioshika utepe ni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Bi. Tonia Kandiero, Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe pamoja na viongozi wengine wa Kitaifa.
Taaswira ya Barabara mpya kutoka Dodoma hadi Fufu Kilomita 70.9 kama inavyoonekana katika picha.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli kushoto akisalimiana na Mwakilishi kutoka Serikali ya Japan na JICA Ndugu Kuniaki Amatsu huku Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania bi Tonia Kandiero akiangalia.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge akiwasalimia wananchi waliofika kwenye sherehe za ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Iringa sehemu ya Dodoma-Fufu(Kilomita 70.9)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wakimtazama Mwakilishi kutoka Serikali ya Japan na JICA Ndugu Kuniaki Amatsu na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania bi Tonia Kandiero walipokuwa wakipanda mti kama ishara ya kumbukumbu ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Fufu(Kilomita 70.9)
Waziri wa zamani wa Ujenzi Mzee Job Lusinde akipanda mti kama ishara ya kumbukumbu ya ufunguzi wa rasmi wa barabara ya Iringa-Dodoma sehemu ya Dodoma-Fufu (Kilomita 70.9) huku Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli , Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge wakishuhudia tukio hilo.
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akiwa amewashika mikono Mbunge wa Dodoma Mjini, David Malole na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Christopher Kangoye huku Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akishuhudia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe akimkaribisha Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Iringa sehemu ya kutoka Dodoma hadi Fufu Kilomita 70.9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli pamoja na viongozi wengine wakitaifa katika picha ya kumbukumbu mara baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma-Iringa sehemu ya Dodoma- Fufu Kilomita 70.9. 

Picha zote kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini –Wizara ya Ujenzi
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: