Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw.Papakiny Kaai akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa NMB baada ya kupokea msaada wa madawati sabini kwaajili ya shule za msingi zilizopo Loliondo
Meneja wa kanda ya Kaskazini Bi.Vicky Bishubo akimkabidhi msaada wa madawati Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw.Papakiny Kaai kwa ajili ya shule za msingi za Loliondo.Kulia ni Meneja wa Huduma kwa wateja katika tawi la NMB Loliondo Bw. Abraham Mbise.

Na Mwandishi Wetu.

NMB imetoa msaada wa Zaidi ya madawati 70 kwaajili ya kusaidia kwa shule za msingi zilizopo wilayani Ngorongoro madawati yote yakiwa na thamani ya Shilingi Milioni 5. Msaada huo unalengo la kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wa shule za Msingi za wilayani Ngorongoro.

Huo ni mwendelezo wa Benki katika kuchangia huduma za kijamii kwa njia ya kurudisha sehemu ya faida inayopatikana kwa wananchi na kuifanya benki kuwa karibu Zaidi na watanzania.

Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini Bi Vicky Bishubo alisema msaada huo ni mwitikio wa NMB kusaidiana na wananchi pamoja na serikali katika kutatua changamoto za uhaba wa madawati kwa wanafunzi wa wilaya ya Ngorongoro.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw.Papakiny Kaai aliishukuru benki ya NMB kwa kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto mbalimbali za wilaya ya Ngorongoro na taifa kwa ujumla hasa katika elimu na afya.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: