Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar
Siku moja baada ya mtoto Happiness Robert kupotea tena katika mazingira ya kutatanisha huko nyumbani kwao Mkuranga, Jeshi la polisi kanda maalum limefanikiwa kumpata mtoto huyo katika bandari ya Dar es Salaam sehemu ya kupandia meli za kwenda Zanzibar.

Jeshi hilo lilimpata mtoto huyo majira ya saa moja na nusu usiku ambapo askari hao wakiwa doria kwenye eneo hilo.

Akithibitisha kuokotwa kwa motto huyo kamanda wa polisi Mkoa wa Ilala Mary Nzuki amesema kwamba kwa mujibu wa askari waliomuokota walipomuhoji mtoto huyo alisema anataka kurudi tena Zanzibar.

Akizungumza mama wa Mtoto huyo amesema kwamba baba wa motto huyo wameachana tangu miaka sita iliyopita na walikuwa katika mgogoro hadi kufikishana katika vyombo vya dola na baada ya hapo ndipo hali hii inayo mkuta mtoto wake kuanza kumtokea.

Aidha Mama huyo amesema kwamba motto huyo amekuwa wa maajabu sana kwake kwani kuna wakati anatembea kama nyoka.

Naye motto huyo amesema kwamba kuna mtu alikuja kumchukua usiku na kumpeleka hapo bandarini na kasha kumtelekeza hapo.

Hata hivyo motto huyo amesema kwamba anahitaji msaada wa kuendelea kusoma.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: