Jiji la Dar es Salaam limekuwa na vibwanga vingi vinavyolifanya lionekana la pekee... Kwa mtu aliyetoka mikoani ni rahisi sana kushangaa na kuona maisha magumu japokuwa wakazi wake wake anasema 'Harudi mtu kijijini, Tunakomaa na Jiji'. Pichani ni baadhi ya vibwanga vinavyoendelea katika jiji hili.
Wengine wameamua kupaki mkokoteni barabarani.
Wengine wameamua kujitafutia ridhiki kwa njia ya kuokota makopo ya platiki.
Foleni ndiyo balaa hili ni eneo la Mivinjeni, Kurasini.
Suala la usafiri nalo huwa ni changamoto kubwa... eneo la Kituo cha Daladala kilichipo eneo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
Wengine hutembea umbali mrefu kuhangaika na usafiri wa kurudi makwao wakati wa jioni...
Mbali na boda boda kukatazwa kuingia mjini ila nao wanakomaa na jiji.
Mfumo wa barabara nao umebadilika... ukiwa umeingia leo jiji hauwezi endesha gari maana utakuwa unatoa macho usijue la kufanya.
Barabara ya Obama nayo ni kichefu chefu kwa foleni wakati wa jioni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: