Mhariri Mkuu Msaidizi wa Jarida ya Euromoney bwana; Duncan Kerr (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa NMB Mark Wiessing (katikati) akipokea chti cha benki bora, kushoto ni mtendaji mkuu wa ukagusi wa ndani wa NMB Augustino Mbogella

Na Mwandishi Wetu.

Jarida la kimataifa la Euromoney la Uingereza limeitaja NMB kuwa benki bora Zaidi kwa mwaka 2014 katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika jijini London hivi karibuni. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa NMB kutajwa kama benki bora Tanzania ambapo mwaka 2013 pia NMB iliibuka kidedea na kutajwa benki bora Tanzania-2013.

Kila Mwaka, Jarida la Euromoney huandaa hafla ya kuyatambua Zaidi ya Makundi 20 ya bidhaa za kitaasisi za kifedha zikiwemo benki kote duniani kwa kuagalia benki bora na ya kiwango cha juu kwa kila bara na benki bora katika nchi takribani 100 duniani kote. Tuzo hii huzitambua taasisi za kifedha duniani kote ambazo zimepata mafanikio ya hali ya juu katika maeneo yao, kwa kuonyesha ugunduzi na kupata mafanikio ya kifedha kila mwaka.

Jopo la wataalam kutoka mataifa mbalimbali na wenye utaalamu mbalimbali hupitia taarifa zinazowasilishwa na taasisi zote za kifedha duniani na kutangaza washindi.

Ndani ya miezi 12, benki ya NMB imeanzisha huduma mbali mbali za kibenki na hivyo kuendelea kuwafikia wateja wa huduma za kibenki kuanzia kuweka akiba, kutoa na kuchukua fedha mijini na vijijini. Kama benki ya kitanzania yenye wateja Zaidi ya milioni 2, Mpango wa NMB unadhihirisha dhamira yake kuhusu elimu juu ya masuala ya kifedha kwa watanzania.” Alisema Mark Wiessing.

“Tunatoa shukrani zetu wa wateja, wafanyakazi na washika dau wote kwa kuwa sehemu ya mafanikio haya makubwa kwa benk, “ alisema Wiessing na kuongeza kuwa NMB itaendelea na ahadi yake ya kuwapa huduma bora wateja wake sasa na siku za mbeleni.

Wiessing aliongeza pia kuwa tuzo hiyo inaongeza kwenye hazina ya tuzo ambazo benki imezipata katika miezi 12 huku akizitaja baadhi kuwa ni benki bora ya mwaka kutoka jarida la Banker, Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wakiipa NMB tuzo ya mlipakodi anaefuata sharia katika taasisi za kifedha nchini. Mwaka 2013 jarida la Euromoney pia liliitaja benki kuwa Benki bora Tanzania huku taasisi ya Super Brand ya Kenya ikiitaja benki bora Tanzania katika taasisi 20 bora Tanzania kwa 2013/3014 na Jarida la the Banker pia liliitaja NMB kuwa benki bora ya kibiashara Afrika Mashariki.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: