Mkurugenzi Mkuuwa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na KilimoTanzaniaBw. Daniel Machemba akiongea na waandishi habari (hawapo pichani) kwenye mkutano wa waandishi kuhusu maonyesho ya bidhaa za Kichina, kushoto kwake ni Mwakilishi wa Uchumi na Biashara kutoka Jamhuri ya Watu China nchini Tanzania Bi.Wang Fang, na kulia kwake ni Bi Rehema Mtingwa Afisa wa Mawasiliano kutoka TPSF.
4.Mwakilishi wa Uchumi na Biashara kutoka Jamhuri ya Watu China nchini Tanzania Bi.Wang Fang akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).

Baadhi ya washiriki waliohudhuria kwenye mkutano wa waandishi kuhusu maonyesho ya bidhaa mbalimbali za Kichina yatakayoanza tarehe 21 hadi 24 mwezi huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania Bw. Daniel Machemba akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China mara baada ya mkutano na Waandishi.

Na Mwandishi Wetu.

China na Tanzania ni marafiki wa siku nyingi na watu wa nchi hizo mbili wanafurahia kuwa na urafiki mkubwa wa jadi. Mawasiliano yameongezeka katika ngazi zote na ushirikiano kwenye sehemu tofauti umepata mafanikio makubwa. Katika miaka hii iliyopita, kutokana na jitihada zilizofanywa na serikali pamoja na kampuni zilizopo katika nchi mbili, ushirikiano wa uchumi na biashara baina ya China na Tanzania umepata maendeleo makubwa. Mwaka 2013, thamani ya biashara kati ya China na Tanzania ilifikia dola za kimarekani bilioni 3.7 ambayo imezidi kwa asilimia 49 kuliko mwaka 2012 na hivyo kuweka rekodi mpya.

Maendeleo ya Tanzania na China ni fursa nzuri kwa pande hizi mbili.Katika miaka ya karibuni, China inaendelea kukuza nguvu za kiuchumi, uvumbuzi wa teknolojia, na hadhi ya maendeleo ya ushirika. Bidhaa kutoka China kwenda nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania zimeendelea kuwa nzuri na zenye bei poa. Wakati huo huo, aina pamoja na ubora wa bidhaa umeongezeka na kiwango cha huduma kimeboreshwa. Imetoa mchango mkubwa katika kukidhi mahititaji ya watumiaji wa Tanzania na nchi nyingine za kiafrika pia katika kuhakikisha ubora wa maisha ya watu na ukuaji wa kiuchumi na kijamii.

Kwa ajili ya kusukuma zaidi uhusiano wa maendeleo ya kiuchumi na kibiashara baina ya China na Tanzania pamoja na Afrika nzima, na kuongeza uelewano wa bidhaa za China katika soko la Afrika, Tukio hilo linafanyika kila mwaka tangu 2012, na linaandaliwa na Idara ya Biashara ya China pamoja na Serikali ya Mkoa(manispaa) inayohusika. Awamu ya kwanza ya Maonyesho ilifanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Sabasaba kuanzia tarehe Juni 29 hadi Julai 3, 2012.Ukubwa wa eneo ni mita za mraba 2600.Na awamu ya pili ina ukubwa wa eneo mita za mraba 5000 ambayo yalifanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee-Dar es Salaam Septemba 10-13, 2013. 

Vikao viwili vilivyopita vimevutia washiriki zaidi ya 300 kwa jumla, kutoka China na kupokea wanunuzi 73,643. Maoneysho yamepata matokeo yanayotarajiwa na sifa ya juu kutoka maeneo ya kisiasa na kibiashara nchini Tanzania.

Maonyesho ya awamu ya tatu itafanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam, Agosti 21-24, 2014, ambalo lina eneo la mita za mraba 5,000. Kampuni zinazojiunga na maonyesho haya zinatoka besi za makundi ya viwanda hasa zikiwemo Fujian, Guangdong , Hebei, Guangxi, Jiangsu, Shandong, Hunan, Shanghai, Chongqing na Zhejiang na watakuja na kuonyesha bidhaa katika makundi mbalimbali ya viwanda. Bidhaa katika maonyesho 2014 yatajitokeza kuonyesha upekee wa mikoa tafauti ili kukidhi mahitaji ya wafanya biashara katika soko mbalimbali. Maonyesho ya 2014 yatajigawanya katika sehemu nne:1,mashine na magari,2,vyombo-umeme vya nyumbani, bidhaa zinazoendeshwa na umeme na nisharti ya jua,3,bidhaa za walaji,4,vifaa vya ujenzi,bidhaa za kemikali,matibabu na yenye matumizi zaidi ya moja.

Maonyesho ya awamu hii mwaka 2014 yataleta kampuni zaidi ya mia moja kutoka mikoa na manispaa kumi na mbili nchini China, zikiwemo kampuni zenye sifa juu ya 500 duniani au makampuni zinazovuma kwa jina kama vile Guangdong Lesso Technology Industrial Co., Ltd., Jiangsu High Hope Group, Shenzhen Yingli New Energy Resources Co., Ltd., Nanjing Automobile Import & Export Co., Ltd., Shanghai Warrior Shoes Co., Ltd. and Shanghai Huayi (Group) Company.

Tunaamini kwamba Maonyesho ya bidhaa za China Afrika itakuwa mojawapo ya majukwaa muhimu ya mawasiliano ya kibiashara na ushirikiano kati ya China na Afrika, ambalo litasaidia kufikisha faida za pande zote mbili na nchi nyingine za Afrika. Itakuza maendeleo mapya ya ushirikiano wa mtindo upya wa kimkakati kati ya China na Afrika chini ya msaada mkubwa wa serikali ya nchi mbili.

Tunawakaribisha sana watanzania wanaoshughulikia kazi za aina mbalimbali kuhudhuria, kuwasiliana na kununua katika Maonyesho ya Bidhaa za China Afrika 2014.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: