Katika kuendeleza wajibu wake wa kutoa mafunzo ya muda mfupi, Chuo cha Diplomasia kimeendesha mafunzo ya juma moja ya Itifaki na Uhusiano ‘PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS’ kati ya tarehe 18 – 22 August, 2014. 

Mafunzo haya yalilenga kuwaongezea uwezo maafisa mbali mbali kutoka serekalini na sekta binafsi. Mafunzo haya ni muendelezo wa mafunzo ya muda mfupi yatolewayo na Chuo cha Diplomasia kila mwezi, katika mafunzo hayo ambayo kwa kawaida wawezeshaji wa mafunzo hayo ya muda mfupi katika Chuo cha Diplomasia, huwa ni mabalozi na wakufunzi waliobobea katika mambo ya Diplomasia na hivyo kuwapa washiriki uzoefu na mafunzo ya kiutendaji zaidi ili kuwajengea uwezo na ufanisi katika kuboresha majukumu yao.

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoa na Balozi Sanga (mwenye Kaunda suti katikati)

Mafunzo hayo yalihusisha maofisa wa kada mbalimbali kutoka idara za Serikali, Chuo cha Ardhi, Jeshi la Wananchi, Magereza, Ubalozi wa Uingereza, na sekta binafsi kama Benki Kuu ya Tanzania, SMART TANZANIA (Telecom), SERENA HOTEL, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Chuo cha Utalii Tanzania, Idara ya Uhamiaji, Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Umoja wa Mataifa (UN),

Mafunzo hayo ya juma moja yaliyofanyika Kurasini Dar es salaam, washiriki walijifunza jinsi ya kuratibu itifaki za dhifa, sherehe za kitaifa na mikutano mingine mbali mbali. Pia walijifunza Diplomasia, uhuisiano wa umma na namna bora ya kuandaa taarifa kwa ajili ya mawasiliano na umma.

Akifunga mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na Kozi fupi, Bw. Juma M. Kanuwa alisisitiza kwamba mafunzo hayo yatawasaidia maofisa hao kuboresha utendaji wa kazi zao.

“Kazi zinazohusiana na itifaki na uhusiano wa umma (Protocol and Public Relations) zinahitaji utaalam ambao utamfanya mtu aweze kutimiza majukumu yake kwa ufasaha na kufikia malengo na matokeo mazuri. Hivyo mafunzo haya ya Itifaki na mengine yote yanayotolewa na Chuo cha Diplomasia yana lengo la kuwajengea uwezo na utaalam washiriki wote ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kupata matokeo bora,” alisema.

Akaongeza kuwa, kutokana na uhitaji mafunzo haya yatarudiwa tena Zanzibar mnamo mwezi wa kumi, yakifuatiwa na ‘INTERNATIONAL SECURITY AND ARMS CONTROL, FRENCH LANGUAGE na DATA COLLECTION AND ANALYSIS (Using SPSS, SQL and STATA) hapa chuo cha Diplomasia, na kuwataka wale wote wanaohitaji wafike chuoni ama kupiga namba 0713667303 au cfrshortcourse@yahoo.com kwa maelezo zaidi na kupewa utaratibu.
Washiriki wa mafunzo kutoka Chuo cha Ardhi na Chuo cha Utalii Tanzania wakipokea vyeti vyao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

4 comments:

  1. daah safi sana, CHUO CHA DIPLOMASIA mpo juu saana kwa kweeli hasa ktk mambo ya protocol, nilishawahi kusoma short course hapo, yaan kama hujaelewa basi huelewi tena mtu ukisoma hapo short course kwani huwa ni za kivitendo zaidi hakuna theories

    ReplyDelete
  2. nawakubali saana chuo cha diplomasia hasa ktk mafunso ya protocol na shortcourse nyinginezo..yaan huwa ni za kivitendo zaidi na lazima uelewe..hongereni

    ReplyDelete
  3. nawakubali saana chuo cha diplomasia hasa ktk mafunso ya protocol na shortcourse nyinginezo..yaan huwa ni za kivitendo zaidi na lazima uelewe..hongereni

    ReplyDelete
  4. hongereni CHUO CHA DIPLOMASIA mimi napenda kusoma hiyo itakayofanyika zanzibar ya protocol and public relations mwez wa kumi....

    ReplyDelete