Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Zaidi ya watanzania 5000 wanatarajiwa kupata ajira kutokana na mtambo wa gesi asilia ambao unaanza kujengwa hivi karibuni.

Imeelezwa kwamba kupitia Mtambo wa LNG viwanda mbalimbali vitakuwepo katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambavyo vitatokana na uzalilisha wa gesi.

Hayo ameeleza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC), Yona Killagane jijini Dar es Salaam ambapo amesema kwamba hadi watanzania wanatakiwa kuanza kuchangamkia fursa hizo mapema ili kuweza kujiinua kiuchumi.

Aidha Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa Uchumi wa nchi unaweza kukua kwa kutumia gesi asili ambapo hadi sasa viwanda 37 vinatumia gesi ambapo vimeweza kuokoa dollar Million 400 katika uzalishaji wao.

Zaidi ya Gesi Asilia trillion 50.5 imegundulika nchini ambapo trillion 42.5 zimetoka katika kina cha kirefu cha majina trillion 8 zimetoka nchi kavu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: