Habari za Uhakika zilizopo mjini Mbeya zinasema kuwa Mwanamuziki wa Injili nchini Tanzania anayejulikana kwa jina la Happy Kamili anayetamba sana na wimbo wake "Mpango Wa Mungu" na "Jina Kubwa" amehukumiwa kifungo cha Miezi Mitatu Jela bila faini katika Mahakama Ya Mwanzo Mkoani humo kwa Kosa la Kusababisha ajali ya barabarani.

Kesi hiyo iliyokuwa imeanza kusikilizwa mwezi January Mwaka huu, siku ya jana imetolewa hukumu kwa Mwanamuziki huyo kupatikana na hatia ya kusababisha ajali kwa kugonga gari lingine kwa nyuma. Mwanamuziki huyo baada ya Kukiri kutenda kosa hilo mahakamani alipatikana na hatia ya Hakimu alitoa Hukumu ya Miezi Mitatu Jela pasipo kutoa Hukumu Mbadala ya Faini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

3 comments:

  1. Huyo hakimu anastahili kufukuzwa kazi kuwa hajui taratibu na mienendo ya adhabu Kuna adhabu mbadala zote hutolewa ili mshtakiwa awe na uwezo wa kuchagua faini au jela

    ReplyDelete
  2. hayo ni masharibu ambayo yamefika bila yeye kutambua,sio kosa la kimakusudi,ni nguvu za giza ambalo lilitaka kujitukuza,pole sana Mungu yuko pamoja nawe.

    ReplyDelete
  3. mh majanga,dar nusu ya madereva tungekuwa jela,kata rufaa

    ReplyDelete