Habari za Uhakika zilizopo mjini Mbeya zinasema kuwa Mwanamuziki wa Injili nchini Tanzania anayejulikana kwa jina la Happy Kamili anayetamba sana na wimbo wake "Mpango Wa Mungu" na "Jina Kubwa" amehukumiwa kifungo cha Miezi Mitatu Jela bila faini katika Mahakama Ya Mwanzo Mkoani humo kwa Kosa la Kusababisha ajali ya barabarani.
Kesi hiyo iliyokuwa imeanza kusikilizwa mwezi January Mwaka huu, siku ya jana imetolewa hukumu kwa Mwanamuziki huyo kupatikana na hatia ya kusababisha ajali kwa kugonga gari lingine kwa nyuma. Mwanamuziki huyo baada ya Kukiri kutenda kosa hilo mahakamani alipatikana na hatia ya Hakimu alitoa Hukumu ya Miezi Mitatu Jela pasipo kutoa Hukumu Mbadala ya Faini.



Huyo hakimu anastahili kufukuzwa kazi kuwa hajui taratibu na mienendo ya adhabu Kuna adhabu mbadala zote hutolewa ili mshtakiwa awe na uwezo wa kuchagua faini au jela
ReplyDeletehayo ni masharibu ambayo yamefika bila yeye kutambua,sio kosa la kimakusudi,ni nguvu za giza ambalo lilitaka kujitukuza,pole sana Mungu yuko pamoja nawe.
ReplyDeletemh majanga,dar nusu ya madereva tungekuwa jela,kata rufaa
ReplyDelete