Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akitambulisha Mhe. Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo kwa Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka siku ya Jumatatu June 9, 2014 Waziri wa Nishati na Madini na ujumbe wake walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ulipo mtaa wa 22, jijini Washington, DC.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akitambulisha Mhe. Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo kwa Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Idd Sandaly siku ya Jumatatu June 9, 2014 Waziri wa Nishati na Madini na ujumbe wake walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ulipo mtaa wa 22, jijini Washington, DC.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akitambulisha Mhe. Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo kwa Mwenyekiti wa tawi la CCM DMV, Ndugu George Sebo siku ya Jumatatu June 9, 2014 Waziri wa Nishati na Madini na ujumbe wake walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani ulipo mtaa wa 22, jijini Washington, DC.
Mkuu wa Utawala na Fedha, Mama Lily Munanka akiongea machache huku akimshukuru Mhe. Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo na Ujumbe wake kukubali kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na baadae kumkaribisha Balozi Liberata Mulamula kutoa maneno machache.
Mhe. Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo akiongea machache na kumshukuru Mhe. Balozi Liberata Mulamula kwa makaribisho mazuri na kuelezea sababu ya ujio wake nchini Marekani ambao alianzia New York kwenye mkutano wa mwongo wa Nishati Endelevu kwa wote (SE4ALL) ambao Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, siku ya alhamisi wiki iliyopita aliuzindua rasmi mkutano uliohudhuriwa na wajumbe zaidi wa 1,000 wakiwamo zaidi ya mawaziri 20 wa Nishati, wafanyabishara, mashirika ya kimataifa yakiwamo ya fedha na Asasi zisizokuwa za kiserikali,
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huu ambao ulianza Juni 4 na kumalizikaJuni 6, uliongozwa na Waziri wa Nishani na Madini Professor Sospeter Muhongo ambaye pamoja na kuhudhuria na kuchangia mijadala mbalimbali, ijumaa ( June 6), alizungumza katika mkutano wa mawaziri kuhusu nafasi ya Nishati katika Ajenda za Maendeleo Endelevu baada ya 2015 na utayari wa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa Bara la Afrika kuhushu Nishati Endelevu kwa wote unaotarajiwa kufanyika mapema mwakani.
Picha ya pamoja ya Waheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo mwenyeji wake Balozi Liberata Mulamula.
Waheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo mwenyeji wake Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Maafisa na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Waheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo mwenyeji wake Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Ujumbe aliokuja nao Mhe. Waziri wa Nishati na Madini kutoka kushoto ni Eng.Jones Olotu(Rural Energy Agency wa Wizara ya Nishati na Madini), Eng. Rwatabangi P. Luteganya (Manager Investment TANESCO), Styden Rwebangila (Energy Engineer Wizara ya Nishati na Madini), Venosa Ngowi (Senior Petroleum Geologist TPDC), Eng. Leonard R. Masanja (Director TANESCO Board of Directors) na Eng. Yahaya I. Samamba (private Secretary to Minister Wizara ya Nishati na Madini)
Waheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo mwenyeji wake Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Wanajumuiya DMV. kwa picha zaidi bofya hapa
Toa Maoni Yako:
0 comments: