Na Saimeni Mgalula, Mbeya
Jeshi la polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu wawili kwa kukutwa na bhangi katika matukio mawili tofauti katika tukio la kwanza jeshi hilo linamshikilia Victor George (38) akiwa mkazi wa Kijiji cha Lupa Wilaya ya Chunya baada ya kukutwa akiwa na kete 15 za bangi zenye uzito wa gramu 75.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa jana majira ya saa 12:50 mchana huko katika kijiji hicho Tarafa ya Kipembawe pia mtuhumiwa ni mtumiaji na mvutaji taratibu za kisheria zinafanywa ilimtuhumiwa afikishwe mahakamani alisema kamanda wa polisi mkoani hapa kamishina msaidizi wa Jeshi hilo Ahmed Msangi.

Na katika tukio la pili anashikiliwa Maneno Msaru (25) Mkazi wa kijiji cha Mabadaga kilichopo Wilaya ya Mbarali Mkoani hapa,baada ya kukamatwa akiwa na kilo 15 na baiskeli tatu aina ya bambucha mali inayodhaniwa ni ya wizi.

Kamanda Msangi akithibitisha tukio hili alisema kuwa mtuhumiwa alikamatwa jana majira ya saa 9:00 mchana kijijini hapo kata ya Chimala Tarafa ya Rujewa Wilayani hapa pia naye alikuwa ni mtumiaji na nmvutaji,vilevile kamanda wa Msangi anatoa wito kwa jamii kuacha kujihusisha na madawa ya kulevya kwani ni kinyume.

Aidha katika tukio jingine la Msako nyara za Serikali Nyama ya Nyati zinashikiliwa na Jeshi la polisi zenye uzito wa kilo 300 zikiwa zina safirishwa kwa kutumia Pikipiki yenye namba za usajili T.494 CDF aina ya T-better.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda Msangi alisema kuwa lilitokea Aprili 29 saa 3 alasiri katika kijiji cha Igawa, Kata ya Lugelele Tarafa ya Rujewa Wilayani Mbarali maeneo ya Barabara kuu ya Mbeya kwenda Njombe na hatimaye Mtuhumiwa alikimbia na kutelakeza pikipiki yake mara baada ya kuwaona askari wa Doria.

Na mwisho Kamanda Msangi anatoa wito kwa jamii kuacha kujihusisha na uwindaji haramu kwani nikinyume na sheria badala yake Wafuate Taratibu zilizopo kwa mujibu wa sheria za nchi pia anawaomba kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo mtuhumiwa wa tukio hilo azitoe iliakamatwe ilisheria zichukuliwe dhidi yake au ajisalimishemwenyewe, alisema Msangi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: