Baadhi ya Wanachama wa Asasi za Kiraia (AZAKI),
---
Muungano wa Asasi za Kiraia Tanzania umeandaa Mdahalo wa wazi kuhusu Changamoto za Mchakato wa Katiba mpya.

Mdahalo huo utafanyika tarehe 31 /5/2014 katika Ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 10.00 Jioni.

Mdahalo huo utatangazwa moja kwa moja na vituo vya ITV, ABM Radio ya Dodoma, pamoja na Chuchu FM na Istiqama Radio za Zanzibar.

Vyombo vingine vya habari vitakavyopenda kuutangaza Mdahalo huu kwa maslahi ya umma pia vinakaribishwa.

Watoa Mada ni waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba: Prof. Mwesiga Baregu na Bw. Awadhi Ally Saidi.

Wananchi wote mnakaribishwa kushiriki katika mdahalo huu ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapata katiba mpya inayokidhi maslahi ya watanzania.

Wote Mnakaribishwa !!!
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: