Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed Mb Dog, amesema baada ya kuachia video yake ya ‘Mbona Umenuna’, anaendelea na juhudi za kuwapatia raha wadau na mashabiki wake kama njia ya kuonyesha makali yake kisanaa.

Mb Dog, pichani.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mb Dog alisema video yake imeandaliwa kwa kiwango cha juu, huku ikiwa ni sababu ya yeye kuendelea kutoa nyimbo nzuri
zinazoonyesha ubora wake.


Alisema kuwa lengo lake ni kufanya makubwa zaidi katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, hasa baada ya kuamua kurudi tena katika soko hilo kwa mikakati ya aina yake.


“Nipo katika harakati za kuonyesha namna gani naweza kuonyesha ubora wangu kama ilivyokuwa mwanzo nilipotoka na wimbo wa kwanza wa Latifa, nikiwa na ‘Madee’.


“Naamini hii ni njia nzuri ya kuwapatia burudani kamili wadau na mashabiki wangu katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya, hasa baada ya kuachia video yangu ya Mbona
Umenuna,” alisema Mb Dog.


Mb Dog yupo kwenye harakati kabambe ya kumrudisha kileleni kwenye sanaa ya Bongo Fleva, akitokea chini ya Kampuni ya Qs Mhonda J Entertainment, yenye maskani yake jijini Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: