Muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front, Moses Kombe, (katikati) na wenzake wakiigiza igizo la kumbukumbu ya Kuwambwa msalabani Yesu Kristo miaka 2000 iliyopita wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika kanisa hilo Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowasa alikuwa ni miongoni mwa waumini waliohudhuria katika ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la KKKT la Azania Front Dar es Salaam.
Waumini wa Kanisa la Kiinjili Tanzania KKKT, la Azania Front la Dar es Salaam wakiwa katika Ibada ya Ijumaa Kuu.
Waumini wa Kanisa la Mtakatifu Joseph wakiwa kwenye ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika leo kanisani hapo.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoriki, Mwadhama Porkap Kadinali Pengo akiubusu Msalaba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam leo.
Waumuni wa Kanisa la Mtakatifu Joseph Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakiwa wanaubusu Msalaba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mtoto, Vanes Mpupua akiubusu Msalaba wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam.
Mmoja wa Watoto waliofika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph akiubusu Msaraba wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu iliofanyika Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: