Meneja wa Kinywaji cha Castle lite,Victoria Kimaro (kulia) pamoja na Meneja msaidizi wa Castle Lite,Geofrey Makau wakionyesha moja ya tiketi za VIP zitakazotumika kwenye  Tamasha kubwa la Msanii TIMBALAND litakalofanyika nchini Afrika Kusini mwanzoni mwa Mwezi Juni.
Meneja msaidizi wa Castle lite,Geofrey Makau akimkabidhi mmoja kati ya washindi wa tiketi ya kwenda nchini Afrika kusini,Bwana Ratifu Gabriel Komba kwa ajili ya kushuhudia Tamasha kubwa la Msanii TIMBALAND litakalofanyika nchini humo mwanzoni mwa Mwezi Juni.
Meneja wa Kinywaji cha Castle lite,Victoria Kimaro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo (hawapo pichani) wakati wa kuwatangaza washindi wa shindano la kwenda nchini Afrika ya kusini kushuhudia Tamasha kubwa la Msanii TIMBALAND litakalofanyika nchini humo mwanzoni mwa Mwezi Juni, Kushoto ni Meneja msaidizi wa Castle Lite,Geofrey Makau.
Washindi wa shindano hilo wakiwa katika picha ya pamoja. 

Meneja msaidizi wa castle lite Geofrey Makau akimkabidhi mmoja kati ya washindi wa Bwana John Jackson Ringo kwenda nchini Afrika ya kusini kushuhudia Tamasha kubwa la TIMBALAND litakalofanyika nchini humo mwanzoni mwa Mwezi Juni.

KINYWAJI cha Castle Lite kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), jana imetaja majina ya Watanzania 12 watakaoshuhudia ‘live’ onyesho la msanii maarufu duniani, Timothy Zachery Mosley aliye maarufu kwa jina la Timbaland.

Onyesho hilo linatarajiwa kufanyika Johannesburg, Afrika Kusini hapo Juni, mwaka huu, huku watu hao 12 wakilipiwa kila kitu ili kushuhudia mambo makali kutoka kwa msanii huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Bia ya Castle Lite, Victoria Kimaro alisema, wanajisikia faraja kupata watu hao waliotokana na promosheni iliyoendeshwa nchi nzima.

Katika promosheni hiyo, wateja na wapenzi wa Castle Lite walitakiwa kutuma namba zilizo chini ya kizibo cha bia hiyo na hatimaye washindi kupatikana kupitia droo iliyofanyika.

“Kwetu kama Castle Lite tunawapongeza s wateja hawa 12 ambao wamefanikiwa kuibuka kidedea katika promosheni hii tuliyoizindua Januari na kumalizika Aprili 4.

 “ Kama tulivyoahidi  wakati wa uzinduzi, washindi hawa wataondoka nchini Juni 6, mwaka huu kwenda Afrika Kusini kushuhudia tamasha hilo.

“Washindi wetu watalipiwa gharama zote za usafiri, malazi, chakula na usafiri wa ndani wakiwa huko na mambo yote haya yatafanywa katika kiwango cha hali ya juu, yaani watachukuliwa kama watu maalumu,” alisema.

Aliwataja washindi hao hao na sehemu wanazotoka zikiwa kwenye mabano kuwa ni, Ratifu Gabriel Komba, William Yobu Msangi, Emmanuel Mathayo Mushi na Amandi Mathayo Kimario ambao wote wanatoka Dar es Salaam.

Wengine ni Bryson Evarist Temu, Gabriel Pankrias Liyakurwa (Kilimanjaro), Kolman Julius Shayo (Mwanza), Fidelis Festus Tesha (Dodoma) na Dickson Ladislaub Kanoni (Tabora).

Wapo pia Dorika Stephania Chirigati, John Jackson Ringo na Frank John Zaburi ambao nao pia wanatoka Dar es Salaam.

Victoria, aliwataka washindi hao kuwa mabalozi wazuri wa Castle Lite muda wote na aliwashukuru wote walioshiriki katika promosheni hiyo.Bia ya Castle Lite inazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: