Kutokana na kukithiri kwa mfumo dume unaoambatana na ukandamizaji wa mwanamke na kusababisha ongezeko la watoto yatima na wajane katika jamii ya wafuagaji wa kimasai, wanawake wa jamii  hiyo wanaoishi ndani  ya eneo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wameunda baraza  la wanawake  litakalosimamia masuala mbalimbali kwa mtoto wa kike husani elimu,afya,na haki ya mwanamke.

Wanawake hao wa jamii ya kimasai wanabainisha kuwa hamasa ndogo ya jamii ya kuwasomesha watotot wa kilke na kutopewa kipaumbele ,afya duni ya jamii hasa mama na motto endapo vitazingatiwa katika jamii hiyo vitasaidia kuondokana na changamoto hizo na hatimae kuongeza idadi ya wasomi hasa watoto wa kike ambao wataikomboa jamii hiyo kwa ujumla .

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza hilo uliofanyika katika makao makuu ya mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro ukienda sambamba na harambee ya kuchangia mfuko wa elimu kwa watoto wa kike  makamu mwenyekiti wa baraza hilo bibi mereyo muresi anasema   litakua chombo muhimu cha kuwasemea wanawake katika vyombo vya maamuzi ndani na nje.


Mhifadhi mkuu wa mamlaka ya ngorongoro  dakta fredy manongi ndiye aliyezindua baraza hilo na kuendesha harambee iliyofanikisha kupatikana kwa zaidi ya shilingi milioni sabini fedha taslimu na
ahadi.


Baraza la wanawake  hao wafugaji linaanzishwa huku tayari kukiwa na baraza la wafugaji ngorongoro ambalo mwenyekiti wa baraza hilo metui ole
shaudo anawaasa  kuwa lengo walilokusudia  la kumkomboa mwanamke
litafikiwa kwa  wao kushirikiana na wadau
wengine
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: