Mbunge wa Viti Maalum kwa vijana kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ester Bulaya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Ester Cup yatakayofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba na uwanja wa Shule ya Msingi Bunda. (Picha na Mpigapicha wetu)
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Mashindano ya soka ya Ester Bulaya ‘Ester Bulaya Cup’ yamezinduliwa rasmi leo kwenye kiwanja cha shule ya msingi Bunda, Mkoani Mara.
Mashindano hayo ambayo mwaka huu yanafanyika kwa mara ya nne mfululizo yanahusisha timu za soka kutoka katika wilaya zote nne za mkoa wa Mara (Rorya, Musoma mjini, Musoma vijini na Serengeti) ambapo yanayaandaliwa na kudhaminiwa na Mbunge wa viti maalum mkoani humo, Ester Bulaya.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mbunge huyo, aisema kuwa msimu wa mwaka huu amefanikiwa kuyaboresha zaidi ambapo zawadi zieongezwa pamoja na timu shiriki kuongezeka kutoka timu 38 mwaka jana mpaka kufikia timu 72 kwa mwaka huu.
Bulaya, alisema kuwa kwa mwaka huu mashindano hayo yatafanyika kwenye wilaya na baadae fainali kufanyika Bunda mjini.
“Kutokana na wingi wa timu, kwa mwaka huu timu kutoka katika Wilaya zote zitashindana huko huko na baadae washindi watakutana Bunda mjini kwaajili ya michezo ya fainali kumpata bingwa wa mwaka huu,” alisema Bulaya.
Alisema kwa mwaka huu zawadi zimeongezeka kutoka Shilingi milioni moja mwaka jana kwa bingwa wa michuano hiyo mpaka kufikia Sh. 1,500,0000 pamoja na kikombe cha ubingwa wakati mshindi wa pili atapata Sh.700,000 na mshindi wa tatu atapata Sh. 500,000.
Kwa mwaka huu mashindano hayo yatatumia zaidi ya milioni 15 kama zawadi, posho kwa waamuzi pamoja na malipo ya viwanja vitakavyofanyikia michezo hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: