Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Bi. Woinde Shisael (kulia) akimkambidhi mfano wa hundi cha kiasi cha Tsh 20,700,000 Kaimu Katibu Mkuu wa Shirika la Red Cross nchini Bi. Bertha Mlay mapema leo katika hafla fupi ya makabidhiano yaliyofanyika makao makuu ya Red Cross, jijini Dar es Salaam. Kiasi hicho kinalenga kuwapatia waathirika wa mafuriko wa Dumila - Morogoro na Dar es Salaam huduma za malazi, maji, chakula, mablanketi, neti za kuzuia mbu na magodoro.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Shirika la Red Cross nchini Bi. Bertha Mlay (katikati) akipokea kwa furaha moja ya mifuko ya sembe kutoka kwa Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Tigo Bi. Halima Kasoro mapema leo. Wafanyakazi wa Tigo waliweza pia kujichanga kiasi cha Tsh 4,000,000 ambayo imesaidia kununua vyakula hivyo.
 Baadhi ya vyakula vilivyotolewa kama msaada na wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Tigo kwa waathirika wa mafuriko wa Dumila - Morogoro na jiji la Dar es Salaam mapema leo.
 Meneja wa Uwajibikaji kwa Jamii kutoka Tigo Bi. Woinde Shisael (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mapema leo wakati wa makabidhiano wa msaada wa fedha na vyakula kwenda kwa waathirika wa mafuriko nchini. Zaidi ya familia 800 zitanufaika na msaada huu, familia 400 kutoka Dumila - Morogoro na 400 wengine kutoka jijini Dar es Salaam. Bi. Shisael pia alitumia nafasi hiyo kuipongeza serikali pamoja na Shirika la Red Cross Tanzania kwa jitihada zao mpaka sasa.
Wafanyakazi wa Tigo katika picha ya pamoja nje ya jengo la Shirika la Red Cross Tanzania, jijini Dar es Salaam mapema leo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: