Wachezaki wa Simba, wakishangilia bao lao la kuongoza lililofungwa na haruna Chanongo.
 Simon Msuva, akishangilia bao lake aliloisawazishia Yanga...
Wachezaji wa Yanga, wakishangilia bao lao la kusawazisha lililofungwa na Simon Msuva.*MATUKIO KATIKA PICHA YA MCHEZO WA YANGA v/s SIMBA NA MATOKEZO YOTE YA MICHEZO YA LEO
 Mshamuliaji wa Yanga, Simon Msumva (kulia) akijaribu kuwatoka mabeki wa Simba, Nassor Chollo (kushoto) na Said Ndemla (katikati) wakati wa mchezo wa kufunga dimba la Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo jioni. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare kwa kufungana bao 1-1. 

bao la Simba walioanza kushinda lilifungwa na Haruna Chanongo, katika dakika ya 76 baada ya Krosi safi ya beki William Lucian. Yanga walisawazisha bao hilo katika dakika ya 86 kupitia winga wake machachari, Simon Msuva, kwa shuti kali lililomshinda kipa Ivo Mapunda. hadi mwisho wa mchezo huo, Yanga 1-1 Simba.

Yanga 1 (Simon Msuva Dk 86') v/s Simba 1 (Haruna Chanongo 76'), 
Oljoro 1 v/s Mtibwa Sugar 1, Rhino Rangers 0 v/s Ruvu Shooting 2 (Hamis Kisuke Dk 10)', Elias Maguli Dk 17')
 Mbeya City 1 (Saad Kipanga Dk 75') v/s Mgambo 0, 
Coastal 0 v/s Kagera Sugar 1 (Themi Felix  Dk 50')
Tz Prisons 1  (Peter Michael Dk 54') v/s Ashanti 0
 JKT Ruvu 0 v/s Azam Fc 1 (Brian Umony Dk 79')
 Kikosi cha kwa nza cha Simba na makocha wake....
 Kikosi cha kwanza cha Yanga...

 Mshambuliaji wa Yanga , Hamis Kiiza akiruka kukwepa kwanja la beki wa simba, Nassor Chollo wakati wa mchezo huo. 
 Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (katikati) akiwatoka wachezaji wa Simba Ramadhan Singano (kulia) na Nassor Chollo.  Picha zote na Sufiani Mafoto.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: