Ukiniambia nikutajie majina matano ya wanamuziki ambao nawaita “vinara” nchini Tanzania,bila shaka kabisa jina la Muhidin Maalim Mohamed Gurumo (pichani) halitokosa.Gurumo ni hazina.Ni mwanamuziki ambaye ana sifa ya pekee ya kudumu katika bendi moja bila kuhama kwa muda mrefu kupita kawaida. Hii ni tofauti kabisa na wanamuziki wengi ambao kila kukicha hubadilisha bendi.

Mwanamuziki huyo alizaliwa Masaki Kisarawe mwaka 1940 na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Sungwi huko huko Kisarawe, na baadae aliacha shule baada ya baba yeke kufariki na kukosa mtu wa kumgharamia mahitaji ya shule.

Baada ya kuacha shule kutokana na kufiwa na baba yake, Gurumo mwaka huo huo alijiunga na bendi ya mtaani iliyojulikna kama Scock Jazz iliyokuwa na maskani yake katika mitaa ya Moshi na Kigoma.



Mwaka mmoja baadae alijiunga na bendi ambayo ilikuwa na vyombo vya kisasa wakati huo, iliyojulikana kana kama Kilimanjaro Chacha, ambako alitunga vibao kama vile Twende Tukalime, Mapenzi Hayana Dawa, Ushirikina ni Sumu na Maendeleo.

Mwaka 1963 Gurumo alijiunga na Rufiji Jazz Band, ambako alitunga kibao cha Uwezo wa Binadamu Kufikiri, ambacho kilimpatia umaarufu mkubwa kufuatia kupenda na wapenzi wengi wa muziki wa dansi.

Baadae mwaka huo huo alijiunga na bendi ya Kilwa Jazz na kutunga kibao cha Wewe Mpenzi Naomba Unishauri Kabla Hatujagombana, na kile cha Siwezi Kukununulia Gari Wakati Hata Baiskeli Sina.







Akiwa na bendi hiyo ya Nuta Jazz, Gurumo alitunga vibao vingi lakini baadhi yake ambavyo alivikumbuka ni Magdalena, Maneno ya Mwalimu Maneno ya Wazee Yote Sawa, Rehema Umefeli Shule kwa Kisa Gani? na vibao vingine.

Baadae bendi hiyo ilibadilishwa jina na kuitwa Jumuiya ya Wafanyakazi, JUWATA, ambapo akiwa na bendi hiyo baadhi ya vibao alivyotunga ni Dada Fatuma, Dada Sabina na vingine vingi kabla haijabadilishwa na kuwa OTTU Jazz Band.
Bendi hiyo imekuwa ikibadilishwa majina kutokana na mmiliki wake, ambao ni Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania, inapobadilisha majina na moja kwa moja bendi hiyo nayo hubadilisha jina lake.

Akiwa OTTU Jazz, jina ambalo hadi sasa wanalitumia, Gurumo baadhi ya vibao alivyotunga ni Tenda Wema na Usia kwa Watoto, ambavyo vimekuwa vikipendwa kila vipigwapo.

Habari kwa hisani ya http://www.bongocelebrity.com/
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments: