Wananchi wakiwa katika taharuki wasijue la kufanya baada ya barabara ya Chalinze Mlanzidi eneo la Ruvu Darajani, Hali hii anatokana na Mvua zinazozidi kunyesha hali iliyopelekea maji kujaa na Kukatiza Juu ya Barabara, kwa usalama magari yote yamesimama kusubiri hali kutengemaa ambapo anasema mpaka hivi sasa saa moja usiku huu hakuna gari lililoweza kuvuka na foleni ni ndefu mno. Wananchi wameamua kukaa kwenye magari yao... huku wengine wamelala baada ya kukata tamaa.
Kila mmoja akipambanua asijue la kufanya.
Wengine waliamua kujipumzisha katika majani....
Foleni mtindo mmoja hkuna cha magari madogo wala mabasi yote yameshindwa kupita baada ya eneo hilo la daraja kujaa maji.
Ripota wa Kajunason Blog, Imani Ntila akiwa eneo la tukio ng'ambo akitokea Morogoro kuja Dar asijue la kufanya baada kushindwa kuvuka. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: