Sehemu ya daraja hilo, linavyoonekana baada ya kuongezeka upana kwa kulika kutoka mita 25 na sasa kufikia mita 75, ambapo tayari Malori yameanza kumwaga vifusi vya mawe ili kuziba eneo hilo na kuweza kuunganisha njia hiyo.
---
Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

Wakazi wa mji wa Bagamoyo na vitongoji vyake wanaotumia daraja la mto Mpiji wapo katika hali tete kutokana na nauli kupanda kutoka shilingi elfu tano mpaka shilingi elfu kumi.

Wakiongea na Kajunason Blog wakazi wa Bagamoyo na vitongoji vyake walisema kwa sasa hali yao ya maisha imepanda kutokana na kukosekana kwa usafiri wa uhakika uliosababisha kupanda kwa nauli.

“Hali ya Maisha kwetu imekuwa mbaya sana, yani kila kitu ni shida kweli… tunaiomba serikali iharakishe kurudisha mawasiliano” walisema wakazi hao.

Kwa sasa nauli ya kutoka Bagamoyo wakati wa asubuhi imekuwa ikianzia shilingi elfu tano (5,000/-) mpaka elfu kumi (10,000/-) na endapo unatoka Dar wakati wa jioni ni shilingi elfu (5,000/-) kwa wale wanaovuka kwa miguu gharama ya kuvushwa ni shilingi 1,000/-

Waliongeza kuwa nauli hizo zimekuja kutoakana na barabara inayotumika ni ile ya kutoka Dar es Salaam unapitia Kibaha na kukatisha kwenda Bagamoyo na ile ya Dar es Salaam kupitia Mbezi Mwisho kwenda bagamoyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: