1Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam inayoandaa matamasha ya Pasaka na Krismas, Bw. Alex Msama anaendelea vizuri baada ya kupata ajali mjini Dodoma kisha kupelekwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika wodi Kibasila namba 16 hivi sasa anaendelea vizuri na amesema hali yake imekuwa ikiimarika tofauti na ilivyokuwa Mwanzo, alisema kwamba Mungu ni mwema na ametenda miujiza yake ndiyo maana amekuwa akiimarika kiafya. (PICHA NA FULLSHANGWEBLOG-MUHIMBILI)2Mfanyakazi wa Kampuni ya Dira, Ally Makuburi akimjulia hali Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Alex Msama ambaye amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, kulia ni Musa Mkama mwandishi wa gazeti hilo pia. 3Mfanyakazi wa Kampuni ya Dira, Musa Mkama akimjulia hali Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Alex Msama ambaye amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya kupata ajali mkoani Dodoma. 5Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Bw. Alex Msama akiwa na wafanyakazi wake naa baadhi ya ndugu na jamaa wakati walipokwenda kumjulia hali katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jana.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: