Meneja wa kinywaji cha Redd's Original, Victoria Kimaro akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya kuzinduliwa kwa
mashindano ya Redd's Miss Tanzania 2014 kulia ni mkurugenzi wa kampuni
ya LINO International Hashi Lundenga ambao ni waandaaji wa mashindano
hayo na kushoto ni Meneja Masoko wa kinywaji cha Redd's Original Vimal
Vaghmaria.
Mkurugenzi wa kampuni ya LINO International, Hashimu Lundenga akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya kuzinduliwa kwa
mashindano ya Redd's Miss Tanzania 2014 katikakati ni meneja wa kinywaji
cha Redd's Original Victoria Kimaro na mwisho ni Meneja Masoko wa
kinywaji cha Redd's Original Vimal Vaghmaria.
Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria kwenye uzinduzi jijini Dar Es Salaam.
---
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original,
pamoja na Kamati ya Miss Tanzania leo wamezindua rasmi kuanza kwa
mchakato wa kumpata “Redds Miss Tanzania 2014/2015.
Akizungumzia
Udhamini wa mashindano ya mwaka huu Meneja wa Kinywaji cha Redds
Original Bi. Victoria Kimaro alisema “Redds Original, ina furaha kubwa
siku ya leo kutangaza udhamini wa mashindano ya kumsaka mrembo
atakayemrithi Happines Watimanywa (Redds Miss Tanzania wa sasa).
Nina
imani wote tunakumbuka kuwa mwaka 2012 Redds ilisaini mkataba na Lino
International wa kudhamini mashindano haya maarufu na yenye hadhi yake
hapa nchini kama mdhamini mkuu kwa kipindi cha miaka mitatu, yaani 2012
hadi 2014, hivyo huu ukiwa ni mwaka wetu wa tatu kwa mujibu wa mkataba,
tunayo furaha kubwa kusema kuwa Redds Original imeweza kutoa mchango
wake kwa jamii ya kitanzania, hususan tasnia hii ya Urembo.” Alisema
Victoria
Akizungumzia
udhamini wa kinywaji cha Redds Original, mkurugenzi mkuu wa Lino
International Bw. Hashim Lundenga alisema; Lino International ina kila
sababu ya kuipongeza Redds Original, kwani zaidi ya kuwa mdhamini mkuu
kwa miaka mitatu kinywaji cha Redds kimekuwa mdau mkubwa wa mashindano
haya kwa miaka mingi. Kwa niaba ya Lino International na wadau wa tasnia
ya Urembo tunawapongeza sana Redds Original kwa imani yao kubwa na
mashindano haya ambayo hakika sasa yanavutia zaidi.
Tuna
imani kubwa kuwa mwisho wa mkataba huu wa miaka mitatu sio mwisho wa
mahusiano mazuri kati ya Lino International, wadau wa Urembo na kinywaji
cha Redds Original.
Aidha
nawataka waandaaji wote wa mashindano haya kuanzia ngazi za vitongoji
hadi kanda kufanya maandalizi mazuri na pia kufanya taratibu kwa
kuzingatia masharti yaliyopo katika mkataba na mdhamini wetu mkuu
kinywaji cha Redd’s pasipo kwenda kinyume.





Toa Maoni Yako:
0 comments: