Kweli Urais hauna ubia wala muda ama sehemu ya kuchapa kazi. Wakati wowote na mahali popote ni sehemu ya kazi, kama inavyoonekana hapa ambako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametulia ndani ya ndege akisafiri kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma huku akiifanyia kazi hotuba yake ambayo ataitoa katika Kikao cha Bunge Maalum la Katiba, Ijumaa, Machi 21, 2014. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amealikwa kuwa mgeni rasmi na kuhutubia Bunge Maalum la Katiba kwa mujibu wa Kanuni 7(1)g na Kanuni 75(1) la ya Kanuni za Bunge Maalum.

PICHA NA IKULU
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: