Tendega akizungumza na wanahabari
Akizungumza
na wanahabari nje ya iliyokuwa kambi ya Chadema mjini Iringa ya CK
Lodge, Tendega alianza kwa kumshukuru Mwenyekiti wa Chadema Freeman
Mbowe na viongozi wengine wote walioshiriki kampeni za chama hicho.
Huku
baadhi ya wafuasi wa chama hicho wakiangua kilio alisema;
“Ninawashukuru makamanda wenzangu na wanaharakati waliokuwa wanapigania
haki Kalenga, wafuasi na wanachama wa Chadema wote, nawapa pole na
hongera kwa kuanza na kumaliza uchaguzi huu uliokuwa na dosari nyingi,”
alisema.
Alisema
maapambano ya ukombozi yana changamoto nyingi na kwamba huo ni mwanzo
wa safari ya mabadiliko makubwa nchini, pale walipokesea mbele ya safari
watajipanga upya.


Toa Maoni Yako:
0 comments: