Mheshimiwa Angellah Kairuki, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, mara baada ya kufungua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa Kampeni ya “Care for Me” – Nijali na Mimi. Mpango huu ni mahsusi kwa ajili ya kuongeza hamasa kwa familia, jamii na Serikali kuhusu wajibu wao wa kutoa malezi, matunzo na ulinzi thabiti kwa watoto wali katika mazingira hatarishi. Katika ngazi zote hapa Nchini. Wengine katika picha ni Bi. Anna Maembe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii Jinsia na Watoto, Viongozi wa SOS Tawi la Tanzania (waliovaa fulana), Bw. Jan-Diter Gosink, Muambata wa Ubalozi wa Ujerumani Nchini na Bi. Yagisa Kolo, Mke wa Balozi wa Uturuki Nchini. Uzinduzi huo ulifanyika katika Kijiji cha SOS kilichopo jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Kairuki kwa niaba ya Serikali akitoa ahadi yake binafsi na ya Serikali kuendelea kulinda na kutetea maslahi ya watoto wanaishi katika mazingiza magumu wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya “Care for Me” – Nijali na Mimi.
Mheshimiwa Kairuki akisoma hotuba yake mbele ya wananchi mbalimbali (hawapo pichani) waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni ya “Care for Me” – Nijali na Mimi.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika Kijiji cha SOS cha jijini Dar es Salaam wakitoa ujumbe wa kuwajali watoto wanaoishi katika mazingira magumu wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya “Care for Me” – Nijali na Mimi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: