Mkurugenzi wa Mipango Mikakati wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB
Development Bank), Jaffar Machano akifungua mkutano huo wa hafla ya
utiaji saini mkataba wa makubaliano.
********

Nwa mwandishi wetu,
Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank) na Benki ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Development Bank of Southern Africa, DBSA) zimeingia mkataba wa 

makubaliano ya kiuwekezaji katika sekta ya uchukuzi nchini jana jioni.


Makubaliano hayo yatasaidia kufufua miundombinu ya uchukuzi ikiwemo Reli ya Kati, Viwanja vya Ndege vya Arusha na Mwanza pamoja na Upanuzi wa Bandari. Zifuatazo ni picha mbalimbali za hafla hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana jioni.
 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development Bank), Peter Noni akizungumza na wadau wakati wa hafla hiyo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (DBSA), Patrick Dlamini akizungumza na wadau katika hafla hiyo.
 Sehemu ya washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Kiserikali,Bunge na Binafsi wakifuatilia matukio ya hafla hiyo.

 Kutoka kushoto ni Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Naibu 
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Ofisa Mtendaji Mkuu wa DBSA, Patrick 
Dlamini, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimali nchini (TIB Development 
Bank), Peter Noni wakifuatilia kwa makini sehemu ya matukio wakati wa 
hafla hiyo.

 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimani nchini (TIB Development Bank), 
Peter Noni (wa pili kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DBSA, Patrick 
Dlamini (wa pili kushoto) wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya 
ushirikiano wa kiuwekezaji katika sekta ya uchukuzi huku ukishuhudiwa na
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia waliosimama) 
na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (kulia waliosimama). Kushoto 
(waliokaa) ni Meneja Mkuu wa Fedha wa DBSA, Bane Makene na Mwanasheria 
wa Bodi ya TIB Development Bank, Martha Maeda (kulia). 

 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimani nchini (TIB Development Bank), 
Peter Noni (wa pili kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DBSA, Patrick 
Dlamini (wa pili kushoto) wakibadilishana nyaraka baada ya kutiliana 
saini mkataba wa makubaliano ya 

ushirikiano wa kiuwekezaji katika sekta ya uchukuzi nchini. Kushoto ni 

Meneja Mkuu wa Fedha wa DBSA, Bane Makene na Mwanasheria wa Bodi ya TIB 


Development Bank, Martha Maeda (kulia).
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe wakizungumza na washiriki wa hafla hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: