Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bw. Adoh Mapunda (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu namna wilaya hiyo inavyoendelea kuboresha huduma za jamii kwa kutumia rasilimali mbalimbali zilizo katika wilaya hiyo.Kushoto ni diwani wa kata ya Kikole Mwl.Haji Mulike na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Bw. Ali Mohamed Mtopa.

Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam.

Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa umesema kuwa utahakikisha rasilimali zote zinazopatikana katika wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na gesi asilia zinatumika kuleta maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bw. Adoh Mapunda wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu uboreshaji wa huduma za jamii kwa kutumia rasilimali mbalimbali zilizo katika wilaya hiyo.

Akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo akiwemo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, watendaji na baadhi ya Madiwani wanaohudhuria kikao kazi jijini Dar es salaam, Bw. Mapunda amesema kuwa halmashauri hiyo imejipanga kupunguza utegemezi wa fedha toka serikali kuu kwa kupanua wigo wa mapato ya ndani kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato.

Amevitaja vyanzo hivyo kuwa vyanzo hivyo vipya ni pamoja na ushuru wa zao la Ufuta ambalo sasa mapato yake yamefikia milioni 595, mauzo ya viwanja na ushuru wa Gesi asilia inayozalishwa katika kijiji cha Songosongo ambayo sasa inatoa asilimia 0.3 ikiwa ni ushuru wa tozo la huduma.

Akifafanua kuhusu mapato hayo Bw. Mapunda amesema kuwa katika zao la ufuta asilimia 20 ya pato hilo inarudishwa vijijini na halmashauri hiyo na kuongeza kuwa mapato ya ushuru wa huduma unaolipwa kwa halmashauri kutokana na shughuli za gesi za kampuni ya PAN AFRICAN ENERGY katika eneo la Songosongo huchangia 20% kwa ajili ya maendeleo ya eneo hilo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: