Mimi binafsi kwa Moyo wa dhati wa kuipenda Nchi yangu ya Tanzania nikubaliane na wajumbe wote walioteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Jakaya M. Kikwete, matumaini yetu kwenu yapo mikononi mwenu juu ya Ujenzi wa mara ya Pili wa Taifa letu tangu Uhuru wetu.

Hofu yangu ni kwa Wanasiasa watakapoingilia mpangilio huu wa Ujenzi wa nyumba yetu Bora Tanzania tuitakayo miaka Miamoja ijayo@..... Watanzania wenzangu kwanini nimeshikwa na Hofu hii kutokana na Mvumo wa Kisiasa ninaousikia kila kukicha hasa kwa CCM na CHADEMA ambao kwa sasa ni vinala wa siasa hapa Nchini kwetu...... Tukumbuke kuwa CCM ni chama Tawala na CHADEMA ni Chama kikuu cha Upinzani, hawa wawili wametulazimisha kuingia kwenye Makundi yao ya Siasa na kutuacha sisi wananchi tukiamini wao ni Tanzania.....

Maombi yangu kwenu wajumbe naomba muwe makini sana na Hawa wanasiasa kwani tumeona wanaanza kutuaminisha kwao kuliko Maslahi ya Taifa letu.... Nikiri wazi kuwa mimi ni Mwanachama wa CCM ambaye naamini chama changu tawala lakini ninaye amini Maslahi ya Taifa kwanza hivyo nachelea kueleza kuwa Endapo wanasiasa watapewa nafasi kubwa basi tutashuhudia ushindi wa Kichama na si ushindi wa Taifa.... Kwani tukumbuke kuwa CCM tuna wabunge wengi sasa kama wajumbe watakubaliana na matakwa ya wanasiasa tutakuwa tumeijenga Katiba ya CCM bila kujitambua kuwa kabla ya ASP na TANU na kuizaa CCM Taifa la Tanzania lilikuwepo toka kuumbwa kwa Misingi ya ulimwengu.

Mwisho niwatakie kila la heri wawakilishi wetu katika kujenga Nyumba yetu ya Tanzania nasi wananchi pasipo kubagua Dini zetu tunawaombea kwa Mungu mpewe Hekima na Busara kwa ajili ya Ujenzi wa Taifa letu imara na Lenye Nguvu.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

Mungu ibariki Afrika na watu wake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: