MENEJA wa NMB Tawi la Madaraka mkoani Tanga,Juma Mpimbi kushoto akimkabidhi Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ummy Mwalimu vitanda saba vyenye thamani ya sh.milioni tano jana ambavyo vimetolewa na Benki hiyo kwa ajili ya wakina mama wajawazito wanapojifungua kwenye halfa iliyofanyika kwenye kituo cha Afya Makorora jijini Tanga,wanaoshuhudia katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Omari Guledi na Mbunge wa Jimbo la Tanga, Omari Nundu.
NAIBU Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ummy Mwalimu akizungumza na wakina mama kwenye kituo cha Afya Makorora Jijini Tanga ambao hawapo pichana mara baada ya kukabidhi vitanda saba kwa ajili ya wakina mama wajawazito wanapojifungua vilivyotolewa na benki ya NMB vyenye thamani ya sh.milioni tano kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego na kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Omari Guledi na anayefuatia ni Meneja wa NMB Tawi la Madaraka mkoani Tanga,Juma Mpimbi. Picha zote na Oscar Assenga,Tanga.
--- 
Na Oscar Assenga wa Tanga.

NAIBU Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu amesifu jitihada zinazofanywa na taasisi za kibenki hapa nchini hasa katika kuisaidia jamii kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo afya na elimu lengo likiwa kuharakisha huduma hizo zinapatikana kwenye maeneo ya wananchi.

Ummy alitoa kauli hiyo jana wakati akipokea vitanda saba vyenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni tano na benki ya NMB kwa ajili ya kujifungulia wakina mama wajawazito katika jiji la Tanga ambapo makabidhiano hayo yalifanyika kwenye kituo cha Afya Makorora jijini Tanga.

Alisema msaada huo umekuja wakati muafaka ambao utawaondolea adha waliokuwa wakiipa wakina mama wakati wa kijifungua na kuwataka kuutumia kwenye matumizi yaliyokusudiwa na sio vyenginevyo.

Aidha aliwataka wakima mama kuwa na utaraibu wa kuhudhuria kwenye vituo vya afya wakati wa ujauzito ili kujua maendeleo yao badala ya kuendelea kukaa majumbani bila kupata matibabu na ushauri kutoka kwa wataalamu.

"Ninayaomba mashiriki mwengine kuiga mfano wa NMB kwa kutumia wajibu wao kuisaidia jamii kwenye masuala mbalimbali ya kijamii "Alisema Mwalimu.

Awali akizungumza katika makabidhiano hayo,Meneja wa Benki ya NMB tawi la Madaraka Mkoani Tanga,Juma Mpitimbi alisema benki hiyo imetoa vitanda hivyo ili viweze kuhudumia vituo mbalimbali vya Jiji la Tanga
ambayo ni sera yake ya kuunga mkono shughuli za kijamii hususani afya ikilenga kupunguza vifo vya akina mama pamoja na watoto.

Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego alisema msaada huo umekuwa ni faraja kubwa sana na hilo tumejidhihirishia kuwa wanawake wakiwezeshwa wanawake kuwaletea maendeleo wananchi katika
maeneo yao.

Dendego alisema wilaya ya Tanga imeweza kuongeza wingi wa matibabu kwa wananchi wake kwa kujiunga kwenye mfuko wa afya ya Jamii CHF ambapo alihaidia uboreshaji wa huduma za afya.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: