Mkurugenzi wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', ambaye pia ni Mjumbe wa Nec CCM, Asha Baraka
amechukua Jukumu la Kumchukua Mtoto wa Marehemu Masoud Mohamed (MCD) aliyezaa na Marehemu Mwantumu. Wote hawa walikuwa wafanyakazi wa ASET kwa miaka mingi japo kila mmoja ameshawahi kuondoka Twanga Pepeta lakini asilimia kubwa Mchango wao ulikuwa katika Bendi Hiyo. 

Mtoto Hussein Soud Mohamed anasoma katika Shule ya Msingi Upanga. Mpiga Gitaa la Bass Jojoo Jumanne ndiye aliyepewa Jukumu la Kumchukua Mtoto huyo na kumpeleka Nyumbani kwa Asha Baraka ambako sasa makazi yake yatakuwa hapo na Atasomeshwa na ASET ili kuenzi Mchango wa Wazazi hawa wawili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: