Baraza la Michezo la Taifa (BMT) linapenda kuufahamisha Umma hasa wapenzi wa Mchezo wa Ngumi za kulipwa kuwa limelazimkka kusitisha mara moja pambano lililotajwa hapo juu kwa sababu zifuatazo:-
A. Promota anayehusika na pambano hilo ndugu jay Msangi ameshindwa kutimiza masharti aliyopewa kufuatia pambano aliloandaa tarehe 30 agusti, 2013 kati ya Francis Cheka na Phil Wiliams kutoka marekani, ambayo ni:-
1. Kulipa madeni yote yanayotokana na pambano la mwaka jana,
- Bondia wa Marekani anadai jumla ya Dola za Kimarekani 8,000
- Waamuzi wa pambano wanadai Tsh. 600,000/-
- Daktari Tshs. 150,000/-
- Gharama za ulingo Tshs. 250,000/-
Hivyo deni la ndani kuwa ni Tshs. 1,000,000/- jumla ya deni lote kuwa ni dola za kimarekani 8,000/- na milioni moja fedha ya kitanzania.
B. Bwana Jay Msangi pamoja na Chama ambacho kimempa ruksa ya kuandaa pambano la tarehe 8 Februari, 2013 wameshindwa kuonyesha mikataba iliyosainiwa kama walivyotakiwa.
C. Baraza limeshindwa kupata uhakika wa fedha za kugharimia pambano hilo kutoka kwa waandaaji kama walivyokuwa wameombwa kuthibitisha uwepo wa fedha hiyo ili kuondoa mgogoro mara baada ya pambano kwa kukosekana malipo kwa wahusika.
Masharti haya yamewekwa kwa makusudi mazima ya kuondoa uwezekano a kuliletea Taifa na Tasnia ya ngumi za kulipwa aibu kubwa kama ile iliyotokea wakati wa pambano la tarehe 30 Agosti, 2013.
Kwa maana hiyo Baraza la Michezo la Taifa (BMT) linamtaka bwana Jay Msangi kama promota wa ngumi za kulipwa kujipanga na kulipa madeni yote yaliyoainishwa hapa kabla ya kuandaa pambano lolote liwe la kitaifa au kimataifa.
Aidha, tunatoa wito kwa vyama au mashirika yote yanayojihusisha na ngumi za kulipwa kuhakikisha kuwa wanafanya kazi zao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zote za mchezo huo kabla ya kuwaruhusu mapromota kuandaa mapambano ili kuepusha migongano na migogoro inayoweza kutokea tu kwa sababu ya kutofuata sheria.
Uamuzi huu umefikiwa katika kikao kizito cha pamoja kati ya BMT, "Tanzania Professional Boxing Federation" ( TPBF ambao ndio wasimamizi wa pambano) "Tanzania Professional Boxing Organization" (waliandaa pambano la tarehe 30 Agosti, 2013) Pugylistict Synticate of Tanzania (PST), Promota Jay Msangi, rais wa TPBC na rais wa Boxing League of Tanzania.
Henry S. j. lihaya
Katibu Mkuu - BMT
06 Februari, 2014
Toa Maoni Yako:
0 comments: