Mkurugenzi wa Blue Sky, Richard Signeski akiongea na waandishi wa haari juu ya ushirikiano wao walioingia na kampuni ya Status Comuunication katika kusambaza kazi za wasanii. Pembeni yake ni Monalisa Shayo ambaye ni meneja mahusiano wa kampuni ya Status Communication.
---
Kampuni ya Status Communication leo imetangaza ushirikiano na kampuni ya usa,bazaji wa filamu ya kimarekani Blue Sky Media ili kuwawezesha kuuza filamu kwenye mitandao ya ITunes, Microsoft, Youtube, Rain na mitandao mingine ya kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Blue Sky, Richard Signeski alisema ushirikiano huu utawafanya watengenezaji filamu kutoka Afrika Mashariki na kati kuweza kuuza filamu moja kwa moja kwenye mitandao mikubwa ya usambaji dunia nzima.
"Lengo la ushirikiano huu ni kuapa watengenezaji filamu kutoka Afrika Mashariki na kati kuweza kuuza filamu zao moja kwa moja kwa watanzamaji dunia nzima" alisema Signeski.
Kwa upande wake, mwakilishi wa Status Communication, Monalisa Shayo alisema ushirikiano wao na Blue Sky ni moja ya tu ushirikiano na makampuni ya kimataifa wanaotaka kuingia katika soko la Afrika Mashariki.
"Mwaka 2013 umekuwa mwaka muhimu kwa Status Communication kwani tumeweza kuingia mikataba na makampuni mbali mbali ili kuweza kuingia soko la Afrika Mashariki" alisema Monalisa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: