Habari na James Melikori, KIA/Picha na Audiface Jackson.
Mzee mmoja aliyetambulika kwa jina la Tulito mkazi wa KIA njia panda ya kuelekea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, mda mfupi uliopita amepata ajali ya kugongwa na gari aina ya fuso pindi alipokuwa akivuka barabara.

Mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa walisikia kishindo cha nguvu ndipo kuangalia mzee Tulito alikuwa tayari ameshagongwa na gari lililomgonga halikusimama. Wasamalia wema waliokuwa karibu na eneo la tukio hawakufanikiwa kunasa walau hata namba za gari hilo, ndipo walipomchukua mzee huyo na kumkimbiza Hospitali ya wilayani Boma kwa matibabu zaidi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: