Wananchi wa wilaya Kinondoni na vitongoji vyake wakiwa wamekaa kusibiria kupewa huduma ya afya iliyokuwa akitolewa bure na Huduma ya Mchungaji Chris Embassy chini ya Mchungaji Chriss aishie na kufanya shughuli zake za kichungaji nchini Afrika Kusini tawi la Tanzania, mwisho mwa wiki katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.
Huduma ya Mchungaji Chris Embassy ya Afrika Kusini ambayo inatawi lake Tanzania mwishoni mwa wiki piliyopita ilitoa huduma za afya kwa wakazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam. Huduma hiyo ya afya ilitolewa ikiwa ni mahususi kwa mchungaji huyo kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa. Pichani ni madokta waliofika kutoa huduma kwa wananchi.
Kila mmoja akipatiwa huduma kwa upole kwa kueleza matatizo yake binafsi.
Baada ya kuwa umepimwa na kupatiwa huduma toka kwa madokta, waliweza kutoa dawa bure... kama ulionavyo dawati la madawa nilivyotayari.
Wananchi wakichangamkia huduma zilizokuwa zikitolewa kiwanjani hapo.
Wananchi wakiwa wamepanga foleni kupata huduma ya afya.
Huduma ya kutoa damu kwa ajili ya kuchangia benki ya damu ilifanyika kwa wananchi kujitoa kikamilifu.
Mmiliki wa mtandao huu nae alikuwa msitari wa mbele kuchangia damu ili kuokoa vifo vya akina mama na watoto pamoja na wale wanaopata ajali.
Toa Maoni Yako:
0 comments: