Dkt. Sengondo Mvungi alizaliwa mwaka 1952 aliwahi kugombea Urais nchini Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 kupitia chama cha NCCR-Mageuzi ambapo alipata jumla ya kura 55,819 sawa sawa na asilimia 0.43% na hivyo kushika nafasi ya 5 miongoni mwa wagombea 10 waliokuwa wanawania uraisi katika uchaguzi huo.
Alikuwa ni msomi na mkufunzi wa sheria aliyebobea. Miongoni mwa vyuo alivyowahi kusoma ni pamoja na
1994: Dr. iur (MCL) Hamburg University
1991: Magister Legum (MCL) Hamburg University
1987: LLM University of Dar es Salaam
1981: LLB (Hons) University of Dar es Salaam
Mpaka anafariki dunia marehemu alikuwa ni Deputy Vice Chancellor (ARC) – University of Bagamoyo, Advocate of the High Court and Court of Appeal of Tanzania, Commissioner for Oaths and Notary Public, Member of the National Executive Council, NCCR – Mageuzi Party.
Mnamo tarehe 3 Novemba, Dr. Mvungi alivamiwa na watu wanaosadikika kuwa majambazi nyumbani kwake Kibamba-Msakuzi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Katika tukio hilo, Dr. Mvungi aliumizwa vibaya hususani maeneo ya kichwani. Alikimbizwa katika hospitali ya Tumbi-Kibaha kabla ya kuhamishiwa Muhimbili kwenye Taasisi ya Mifupa kabla ya kuhamishwa tena kwenda Milpark Hospital iliyopo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Mapema jana, Waziri wa Mambo Ya Ndani, Dr. Emmanuel Nchimbi alitangaza kwamba jumla ya watu 9 wanaosadikika kuhusika na tukio hilo la uvamizi kwa Dr.Mvungi wamekamatwa na kwamba taratibu zinafanyika kuwafikisha mahakamani. Bila shaka makosa yaliyokuwa yakiwakabili yataongezeka kutokana na kufariki dunia kwa Dr.Mvungi.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.Pole nyingi kwa ndugu,jamaa na marafiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments: