JESHI LA POLISI VISIWANI ZANZIBAR, LIMEKAMATA SHEHENA KUBWA YA MENO YA TEMBO YALIYOKUWA YAKISAFIRISHWA KWENDA NCHINI UFILIPINO KWA NJIA ZA MAJINI.
MENO HAYO AMBAYO YAMEKAMATWA KWA USHIRIKIANO WA MAKACHERO WA POLISI WA KIMATAIFA INTERPOL HAP[A NCHINI, NI VIPANDE 1021 VYENYE UZITO WA KILO 2915 YAKIWA YAMECHANGANYWA PAMOJA NA VIUMBE VYA BAHARI KATIKA MAGUNIA 98.
AFISA HABARI MKUU WA JESHI LA POLISI ZANZIBAR INSPEKTA MOHAMMED MHINA, AMESEMA SHEHENA HIYO AMBAYO ILIKAMATIWA BANDARIONI IKIWA TAYARI KUSAFIRISHWA KWENDA NJE YA NCHI NI YAPILI KUKAMTWA VISIWANI HUMO AMBAPO MWAKA 2011 MENO YA TEMBO YENYE UZITO WA KILO 1055 YALIYOKUWA YAKISAFIRISHWA KWA MAGENDO KWENDA NJE YA NCHI KWA NJIA ZA MAJINI.
WAZIRI WA MALIASILI NCHINI BALOZI HAMISI KAGASHEKI AKIFUATANIA NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS ZANZIBAR MH. HAJI OMARI KHERI, WALIFIKA KATIKA BANDARI YA ZANZIBAR KUSHUHUDIA SHEHENA HIYO YA MENO YA TEMBO NA KUWAPONGEZA POLISI KWA JUHUDI ZAOO KATIKA UFUATILIAJI WA NYENDO ZA MTANDAO WA MAJANGILI WA KIMATAIFA.
AKIZUNGUMZA NA WANDISHI WA HAABARI BANDARINI HAPO, WAZIIR WAZIIR KAGASHEKI SERIKALI INAENDELEA KUFUATILIA MTANDAO HUO ILI KUUTOKOMEZA NA KUWANUSURU TEMBO WETU HAPA NCHINI.
NA KWA UPANDE WAKE WAZIRI WA NCHI AFISI YA RAIS IDARA MAALUM MHE HAJI OMAR KHERI AMEMSMA SERIKLAI ITACHUKUA HATUA KALI DHIDI YA WALE WALIOHUSIKA NA USAFIRISHAJI WA MENO HAYO.
NAYE KAMISHNA WA JESHI LA POLISI ZNAIZBAR CP MUSSA ALI MUSSA AMEMSMEA POLIS IMEKAMA TA WATU WAWILI WAZALENDO NA IANENDELEA KUWAHOJI NA KUFANYA UPEKUZI NJE YA BANDARI PAMOJA KWAMBA TAARIFA ZINAONYESHA KUWA MZIGO HUO NI WA RAIA WA CHINA.
Toa Maoni Yako:
0 comments: