Paul Okoye wa kwanza kulia, akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu tamasha watakalolifanya kesho Jumamosi. Novemba 23 katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Peter Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P Square, wakiwa na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa ambao ni wadhamini wa wasanii hao pamoja na Lady Jay Dee mmoja wa wasanii watakaowasindikiza jukwaani wasanii hao.
Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule akipeana mkono na wasanii, Peter na Paul Okoye, maarufu kama P Square wakati walipowasili kwenda kutoa msaada katika kituo cha watoto wenye ulemavu wa usonji “Autism” (utindio wa ubongo) cha Msimbazi Mseto, jijini Dar es Salaam.
.Msanii Peter Okoye akimuweka vizuri katika bembea mmoja wa wanafunzi wenye ulemavu wa usonji katika shule ya Msimbazi Mseto jijini Dar es Salaam. Wa kwa nza kutoka kushoto ni mwalimu Mkuu wa shule hiyo Reuben Gadi na Mjumbe wa bodi ya shule hiyo Mtumwa Nindi, na wa kwanza kulia ni mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Precious Hughes ambao ni wadhamini waliofanikisha wasanii hao kutua nchini.
Wasanii wa kundi la P Square (Peter na Paul Okoye) katikati wakimsikiliza Mtoto mwenye ulemavu wa Usonji, Erick wa shule ya msimbazi Mseto walipokwenda kushiriki kutoa msaada kwa kituo cha watoto hao. Wa kwanza kushoto ni mwalimu mkuu wa shule hiyo Reuben Gadi na kulia ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo.
Wasanii wa kundi la P Square wakikabidhi misaada mbalimbali kwa watoto wenye ulemavu wa usonji wa kituo cha Msimbazi Mseto cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule akishuhudia makabidhiano hayo, na katikati ni walimu wa shule hiyo wakipokea kwa pamoja misaada hiyo.
Wasanii Peter na Paul Okoye Maarufu kama P square wakiwa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha huduma za jamii Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule wakicheza pamoja na watoto wenye ulemavu wa usonji wa shule ya msingi ya Msimbazi mseto, wakati waliposhiriki kutoa msaada katika shule hicho kwa watoto hao wenye mahitaji maalum.
· Waviomba kuwapa ushirikiano wasanii wa muziki nchini
· kufanya onesho kwa masaa mawili mfululizo
· Washiriki katika shughuli za kijamii
Baada ya kuwasili nchini usiku wa jana wanamuziki mapacha Peter na Paul Okoye maarufu kama “P – Square” wametoa wito kwa vyombo vya habari nchini kuwasaidia wasanii wandani na kuwa chachu ya mafanikio ya muziki kama vilivyo vyombo vya nchi nyingine, huku wakiahidi kufanya makubwa katika Shoo yao ya siku ya leo kwa mashabiki wao watakaojitokeza katika Viwanja vya Leaders Club.
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hotel ya Hyatt jijini Dar wasanii hao wamesema wamefurahishwa na mapokezi waliyoyapata kutoka kwa jamii ya Watanzania na waandaaji wa Tamasha hilo na kuahidi burudani ya kipekee kwa Watanzania.
Peter Okoye ambaye ni mdogo wake na Paul alisema, vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuwajenga wasanii huku akitoa wito kwa vyombo hivyo kuwa kichocheo cha kuwajenga wasanii na sio kuwabomoa.
“Vyombo vya nchini kwetu vimetufikisha hapa tulipo wamejitahidi kutujenga na kutusaidia kusikika Afrika nzima., Tutaona fahari kama vyombo vya hapa nchini pia vitajenga uwezo wa kuwasaidia wasanii wa ndani nao waweze kufika au hata kuzidi hapa tulipo, Tutafurahi siku tukiwaona wasanii kama kina Jay dee na Ben Pol wakija Nigeria kama sisi tulivyokuja nchini kwao, alisema Paul.
Paul Okoye ambaye ni kaka kwa Peter amesema “Tumefurahishwa sana na mapokezi tuliyoyapata tangu jana usiku hadi kufikia sasa, tumejisikia faraja kuwa katika nchi hii ya Tanzania watu wake ni wakarimu sana sifa hizi tumezisikia kwa watu mbalimbali na tumeshuhudia wenyewe tunawaahidi Mashabiki wetu kufanya Shoo ya uhakika., alisema Paul Okoye.
Kwa upande wa wadhamini wakuu wa Tamasha hilo Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa,alisema wamejisikia faraja kwa pamoja kufanikiwa kuwaleta wasanii hao ili watoe burudani kwa Watanzania na kuweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kutoa msada wa vyakula katika shule ya Msingi Msimbazi Mseto kwa kupitia mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom” Vodacom Foundation”.
“Kwa upande wetu sisi kama waandaaji kila kitu kimekamilika kuanzia, masuala ya usalama na jukwaa vyote vimekamilika, Pamoja na mambo mengine tunatoa wito kwa Watanzania kuwai kufika maana onyesho litaanza saa 1 na kuwa sihii kuwa wastaarabu wakati wote wa Shoo hiyo na kujiepusha na vitendo vyovyote ambavyo vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Wasanii kutoka Bongo watakao toa burudani katika Tamasha hilo ni pamoja na wakongwe, Prof. Jay, Lady Jaydee, Jo Makini”mwamba wa kaskazini”pamoja na Ben Pol.
Wakati huo huo wasanii hao na kitengo cha huduma za jamii cha Vodacom Foundation wameshiriki katika kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wenye ulemavu wa akili cha Msimbazi Mseto kilichopo jijini Dar es Salaam. Huku wakitoa wito kwa jamii ya Watanzania kuendelea kuwasaidia watu wote wasio na uwezo ili kujenga jamii yenye maisha sawa kwa wote.
Toa Maoni Yako:
0 comments: