Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Benchmark, Evelyn Byaruhanga akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na fainali za shindano la Epiq BSS zitakazofanyika tarehe 30 katika ukumbi wa Escape 1. Kulia kwake ni Arnold Madale, mtaalamu wa Chapa mkuu kutoka Zantel. na kushoto ni mmojawapo wa washiriki, Amina Chibaba.
Mshiriki Amina Chibaba akiimba wimbo wake mbele ya waandishi wa habari wakati wa kutangaza fainali za shindano hilo zitakazofanyika tarehe 30 pale Escape 1. Kulia kwake ni Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Benchmark, Evelyn Byaruhanga na anayefuata ni Arnold Madale, mtaalamu wa Chapa mkuu kutoka Zantel.
Mshiriki Elizabeth Mwakijambile akiimba wimbo wake mbele ya waandishi wa habari wimbo wake mpya wakti wa kutangaza fainali za EBSS zitakazofanyika Nov 30 pale Escape 1. Kushoto kwake ni Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Benchmark, Evelyn Byaruhanga na anayefuata ni Arnold Madale, mtaalamu wa Chapa mkuu kutoka Zantel.
Mshiriki Emanuel Msuya akiimba wimbo wake mbele ya waandishi wa habari wakati wa kutangaza fainali za shindano hilo zitakazofanyika tarehe 30 pale Escape 1. Kulia kwake ni Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Benchmark, Evelyn Byaruhanga na anayefuata ni Arnold Madale, mtaalamu wa Chapa mkuu kutoka Zantel.
Mshiriki Melisa John akiimba wimbo wake mbele ya waandishi wa habari wimbo wake mpya wakti wa kutangaza fainali za EBSS zitakazofanyika Nov 30 pale Escape 1. Kushoto kwake ni Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Benchmark, Evelyn Byaruhanga na anayefuata ni Arnold Madale, mtaalamu wa Chapa mkuu kutoka Zantel.
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja
---
Baada ya miezi mitatu ya burudani ya kipekee fainali za shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search zitafanyika tarehe 30 kwenye ukumbi wa Escape 1, Mikocheni kuanzia saa moja usiku.
Mpaka sasa wamebaki washiriki sita, Melisa John ambae namba yake ya kupigiwa kura ni 22, Amina Chibaba (03), Emmanuel Msuya (21), Maina Thadei (15), Mandela Nicolaus (10) na Elizabeth Mwakijambile (08), ambapo mshiriki mmoja atatoka ili kubakiza washiriki watano wataoingia fainali.
Tofauti na miaka iliyopita, mwaka huu siku ya fainali, washiriki wataimba nyimbo zao wenyewe, ambazo wamezirekodi tayari, kupitia studio za Mkubwa na Wanae chini ya mtayarishaji Shirko, Burn Records chini ya Shedy Cleva pamoja Fishcrab ya Lamar.
Akizungumzia sababu ya kuwarekodia mapema washiriki, Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Benchmark, Evelyn Byaruhanga alisema wanataka mashabiki wawatambue mapema kabla hawajaingia kwenye muziki rasmi.
‘Kama sote tunavyojua, kutoka kwenye muziki sio kazi ndogo, kwa hiyo ndio maana EBSS mwaka huu imeamua kuwarekodia washiriki waliongia fainali wimbo ili mashabiki wawajue mapema’ alisema Ritha.
Nyimbo hizo zitazinduliwa kwa mara ya kwanza siku ya fainali, tofauti na miaka ya nyuma ambapo washiriki wamekuwa wakiimba nyimbo za wasanii wengine huku mshindi akiondoka na shilingi milioni 50 kutoka kampuni ya simu ya Zantel.
Akizungumzia fainali hizo Evelyn Byaruhanga alisema maandalizi yanaendelea vizuri, na kuwaomba watanzania wengi wajitokeze kutazama fainali hizo pale Escape 1 Mikocheni.
‘Pamoja na washiriki kutoa burudani kali siku hiyo, pia tumewandalia burudani nyingine nyingi na za kipekee, na hii yote ni kuwaonyesha kuwa shindano hili ni zaidi ya mashindano bali ni burudani pia’ alisema Ritha.
Madam Ritha alisema shindano bado halijafungwa kwani wapenzi wa shindano hilo wanatakiwa kuendelea kumpigia kura mshiriki wanayempenda ili aibuke mshindi wa milioni hamsini pamoja na mkataba wa kurekodi.
Kwa upande wake mtaalamu wa Chapa mkuu kutoka Zantel Arnold Madale, alisisitiza umuhimu wa watanzania kumpa ushirikiano mshindi hasa kwa kuwa shindano hili linaamuliwa kwa kura zao.
‘Kwa miezi sita iliyopita Zantel kwa kushirikiana na Benchmark tumewekeza raslimali pamoja na juhudi kubwa ili kuhakikisha Epiq Bongo Star Search inatoa mshindi ambaye atakuwa staa wa kweli’ alisema Khan.
Fainali za mwaka huu zitasindikizwa na Barnaba Boy, Walter Chillambo, Peter Msechu, Snura wa Majanga, Shaa pamoja, Young Killer, Makomando na Borabora Band.
Kiingilio kwa wageni maalumu (VIP) ni shilingi 50,000, ikujumuisha vinwyaji, huku kawaida ikiwa ni shilingi elfu 20,000.
Toa Maoni Yako:
0 comments: