Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Rapper Cindy Rulz anazidi kufanya vizuri Worldwide. Muziki wake unazidi kusambaa katika wigo wa Dunia sasa, sio Afrika tu. Uwezo wake wa kuchana kwa lugha ya Kingereza na Kiswahili unamnyooshea wigo huo pia.
Ni juzi kati tuu mrembo huyo aliyebarikiwa kipaji cha kurap vizuri aliachia wimbo wake mpya ambao amemshirikisha Producer Dunga. Wimbo huo umepewa jina la Lets Wait na ulitengenezwa kwenye studio za Fishcrab cookout.
Lets Wait ni wimbo mzuri sana kiasi cha kufanya baadhi ya mashabiki wa Cindy Rulz kuhisi kuwa huo ni wimbo mkali kuliko zote alizowahi kufanya. Pongezi liende kwa Producers, Lamar na Dunga ambao kwa kiasi kikubwa pia wamefanya wimbo huo kufika levels ilipo sasa.
Kwanza kabisa Lyrics za wimbo huo zimekuwa certified na Rapgenius, kwa maana hiyo mashairi ya wimbo huo yanapatikana kwenye website kubwa ya mashairi nchini Marekani, Rapgenius.com ambayo inatembelewa na mamilioni ya watu kila siku.
Mtu wa kwanza hapa Bongo kusikia akiwa amewekewa mashairi kwenye mtandao huo ni Gosby, sasa Cindy Rulz nae amemanage kufika huko na naamini hizo ni juhudi binafsi ili kuweza kufikisha wimbo katika level za kimataifa. Naamini watu kutoka sehemu mbalimbali duniani wanasoma mashairi ya Lets Wait na kusikiliza audio so that they can sing along at the same time kwasababu mtandao huo unaruhusu kufanya hivyo.
Sasa katika katika pitapita zangu nikakutana na blog moja, Death Chambers Music ya Marekani ikiwa inauzungumzia wimbo huo huo wa Lets Wait. Mwandishi wa habari hiyo alikiri kwamba haelewi moja kwa moja kilichozungumziwa kutokana na mchanganyiko wa lugha, Kingereza na Kiswahili ila aling'amua kwamba kinachozungumziwa ni mapenzi. Lakini mwandishi huyo pia hakuweza kujizuia kumsifu Cindy Rulz kwa jinsi
alivyoweza kupita vizuri kwenye beat ya wimbo huo.
Anyways, Cindy hakuishia hapo kwani siku chache baada ya kurelease wimbo huo mpya akaachia video ya wimbo wake uliopita, Utanifanya Nighairi ambao amemshirikisha Chidy Bway. Ngoma ilifanywa pale G. Recs kwa KGT, honestly naukubali sana huu wimbo.
Kitu kizuri kuhusu hii video ni jinsi ilivyopokelewa vizuri na mashabiki wa muziki wa Bongo Flava. Lakini kizuri zaidi ni pale mtandao mkubwa wa Marekani tena viewhiphop.com kuupromote au kuupa shavu kwa kuitupia video hiyo kwenye mtandao wao, bonge la zali sio? Naamini ukiwa na juhudi binafsi kama msanii lazima utafika mbali tu.
Cindy Rulz ni msichana anayejua kurap na anafanya muziki mzuri, mwenyewe anakwambia classic music, yuko serious na anachokifanya na yupo kwenye management nzuri pia. So naamini juhudi zake zitamfikisha mahala anapopataka, atakuwa msanii wa kimataifa kama anavyojijenga sasa.
Haya ni mafanikio ambayo wasanii wengi wa Bongo hawayapati na matokeo yake wanaishia kusikika hapa hapa nyumbani. Mafanikio haya pia yanarahisisha collabo na wasanii wakubwa duniani kwa sababu muziki wako utasikilizwa na watu wengi wa nchi tofauti tofauti na kufanya muziki wako kukua zaidi.
Kwa hapa nyumbani, Cindy Rulz amepata Interviews zakutosha karibu kwenye Radio zote za Dar es Salaam na TV stations tangu ameachia audio na video za Lets Wait na Utanifanya Nighairi respectively.
Hongera Cindy, now you are rocking on Keezywear.com na endelea kuwakilisha muziki wa Tanzania duniani kote! Endelea kurequest nyimbo za Cindy Rulz on your favorite Radio na TV!
Like Keezywear on Facebook!
Follow @keezywear on Twitter!
Toa Maoni Yako:
0 comments: