Hivi karibuni msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania, Naseeb Abdul a.ka. Diamond alionekana katika picha mbali mbali akiwa amehudhuria sherehe ya harusi ya Msanii anayeunda la kundi la P-Square, Peter Okoye jambo ambalo limeonyesha kuwa alizamia tu.

Kwa mujibu wa msanii huyo Peter Okoye amesema kuwa Mwanamuziki wa P-Square, Peter Okoye ameoneshwa kushangazwa na taarifa kwamba mwanamuziki wa bongo fleva Naseeb Abdul alihudhuria harusi yake hivi karibuni nchini Nigeria na kuhudhuriwa na mastaa mbali mbali akiwenmo msukumba gozi wa Totenham Hotspurs Adebayor.
Awali kupitia blogs mbali mbali kulisambaa taarifa kuwa Diamond alikua mwanamuziki pekee Afrika Mashariki aliyealikwa katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na tajiri nambari wani Afrika, Aliko Dangote.

Blogs hizo zilikwenda mbali kwa kumpamba Diamond kwa vyeo vya ajabu ajabu ikiwemo Michael Jackson wa afrika mashariki jambo ambalo lilisababisha wengi kumponda.

Akihojiwa na kituo cha EATV hivi karibuni mara baada ya kuwasili jijini Dar kwa ajili ya shoo iliyopigwa viwanja vya leaders club, Okoye alishangazwa na taarifa za Diamond kuhudhuria katika harusi yake.

Okoye alikua akijibu swali aliloulizwaa na mtangazaji wa kipindi cha HotMix Adrian Hilary kuhusu Diamond kuhudhuria harusi hiyo ambapo alionesha kushangazwa na jina hilo na kuhoji Diamond ni nani?
Kushangaa huko kulimaanisha licha Diamond kucheza mbele ya Okoye siku ya harusi yake lakini mwanamuziki huyo hakuwa akijua aliyekua akimzungushia viuno vya ngololo ni nani.

Jambo lingine ambalo linaonyesha kuwa wasanii hao hawakuwa akimtambua Diamond ni baada ya kuanza kutoa shukrani zao, waliwataja wasanii watatu tu ambao kiukweli ni dhahili ilionyesha hafahamiki. 

"Thanks to Proffeser J, Lady Jay Dee and AY... Hizo ndizo shukrani zao kwa akili ya haraka haraka kama walikuwa wakimtambua Diamond kuwa yupo nchini kwao Nigeria kwa nini alishindwa hata kumtambua? Au zilikuwa ni dharau? Kwao...."

Kikubwa tunachotaka ni msanii Diamond kuweka wazi je alikuwa ni mzamiaji tu au kuna mengine yalikuwa yametokea...
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: