Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa Bi.Herieth Koka(kushoto)akimpatia  mmoja wa wateja keki aliefika dukani hapo ikiwa ni ishara ya kuendelea kusherehekea na kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja nchini.
 Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimfanyia mahojiano Afisa Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Bi.Herieth Lwakatare,kuhusiana na kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Bw.Rene Meza akisalimiana na baadhi ya wateja waliofika kupata huduma mbalimbali Vodashop Mlimani City na kupata frusa ya kujumwika na Mkurugenzi huyo katika kusherehekea na kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja nchini.
 Mfanyakazi wa Vodashop Mlimani City Bi.Charity Kalima,akiwa na furaha kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake kwa kipindi hichi cha kusherehekea na kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja nchini.
  Mkuu wa Idara ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Brigita Stephen akiwafafanulia jambo baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya waliotembelea makao makuu katika kusherehekea na kuadhimisha  wiki ya huduma kwa wateja nchini.
 Afisa Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Bi.Herieth Lwakatare(katikati)akipozi kwa picha na wafanyakazi wenzake.
Washindi wa zawadi ya huduma bora kwa wateja wa ndani waliochaguliwa na Idara ya Mahusianao na Mawasiliano na Idara ya Wateja wa Mikataba Zenobius Mlowe (kulia) kutoka idara ya manunuzi na Faraji Hiza (kulia) wa idara ya Huduma kwa Wateja wakiwa na tuzo zao katika picha ya pamoja na wasanii wa kike wa kizazi kipya mara baada ya kukabidhiwa tuzo zao katika hafla fupi iliyofanyika kwenye idara ya Mahusiano na Mawasiliano ya Vodacom Makao Makuu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: