Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mh. Haji Hemed akiongea na wakazi wa Kijiji cha Lukozi wilayani humo wakati wa msafara wa “Tigo Smile Tour.” Akiongea na wakazi hao alisema anaipongeza kampuni ya Tigo kwa kuzidi kuwekeza na kuongeza wigo wa mtandao wao nchi nzima.
Wakazi wa Kijiji cha Lukozi wilayani Lushoto wakimskiliza Mkuu wa Wilaya hiyo Mh.Haji Hemed wakati msafara wa “Tigo Smile Tour” wilayani hapo mwishoni mwa wiki.
Kikundi cha sarakasi kikitoa burudani kwa wakazi Mwenge jijini Dar es Salaam wakati wa msafara wa “Tigo Smile Tour” msafara unaopita mikoa 23 na kata 204 huku ikizindua minara 209 mipya ambayo kampuni Tigo imewekeza nchi nzima.
Msanii wa bongo fleva Hamad Ali a.k.a Madee akiwaburudisha wakazi wa Mwenge jijini Dar es Salaam wakati wa msafara wa “Tigo Smile Tour” ulipotembelea eneo hilo.
Mtoto ambaye jina lake halikupatikana akifurahia kuteleza kwenye mchezo wa kuruka kwenye pulizo (jumping castle) wakati wa msafara wa “Tigo Smile Tour” ulipotembelea Mwenge jijini Dar es Salaam.
Wakazi wa Mwenge jijini Dar es Salaam wakipata burudani ya nguvu toka kwa msanii Hamad Ali a.k.a Madee wakati msafara wa “Tigo Smile Tour” uliposimama eneo hilo.








Toa Maoni Yako:
0 comments: