Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Oktoba 24, 2013 ametembelea na kukagua Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma kujionea maandalizi ya jinsi Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba watakavyokaa katika Ukumbi wa Bunge hilo. Bunge hilo Maalum la Katiba litakuwa na Wabunge 600 tofauti ya Bunge la sasa lenye Wabunge 354 ambao ni pamoja na Wabunge 239 wa kuchaguliwa kutoka majimboni, Wabunge Wanawake Viti Maalumu 102, Wabunge wa kuteuliwa toka Baraza la Wawakilishi Zanzibar 5, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wabunge 7 (kati ya 10) wa kuteuliwa na Rais.
Rais Kikwete akikaribishwa kutembelea Jengo la Bunge mjini Dodoma na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai leo Oktoba 24, 2013
Rais Kikwete akiangalia sehemu ya viti ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013
Rais Kikwete akitembelea Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013
Rais Kikwete akizungumza na Naibu Spika Mhe Job
Ndugai na Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila baada ya
kutembeleaUkumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013
Rais Kikwete akisindikizwa na Naibu Spika Mhe Job Ndugai na Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila baada ya kutembelea Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013
PICHA NA IKULU
Toa Maoni Yako:
0 comments: