TIMU ya Yanga SC leo imefikisha jumla ya Pointi 12 na kupunguza pengo la pointi dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kupanda hadi nafasi ya pili baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 2-0 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Simba SC inaendelea kushikilia usukani wa Ligi hiyo ikiwa na pointi 15, baada ya timu zote kucheza mechi saba.
Pasi ndefu ya Athumani Iddi ‘Chuji’ ilimilikiwa vyema na Mrisho Khalfan Ngassa, ambaye kama kawaida yake alimzidi maarifa beki Salvatory Ntebe kabla ya kufumua shuti na kumchambua kipa Hussein Sharrif ‘Casillas’ dakika ya sita.
Mrisho Ngassa tena alimtoka vyema beki wa pembeni wa Mtibwa, Paul Ngalema na kutia krosi maridadi iliyounganishwa vyema na Didier Kavumbangu dakika ya 24 na kuandika bao la pili.
Kipindi cha pili, Mtibwa walirudi wakiwa imara zaidi na kuonyesha upinzani kwa Yanga, wakijitahidi kuwadhibiti vizuri washambuliaji wa timu hiyo na pia kushambulia.
Hata hivyo, uimara wa safu ya ulinzi ya Yanga iliyoongozwa na mchezaji bora Tanzania, Kevin Yondan uliinyima Mtibwa japo bao la kufutia machozi.
Katika mchezo huo, kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite/Juma Abdul dk77, David Domayo, Didier Kavumbangu, Mrisho Ngassa na Hamisi
Katika mchezo mwingine, Mgambo JKT imefungwa nyumbani 1-0 na Prisons Uwanja wa Mkwakwani, Tanga bao pekee la Peter Michael dakika ya 62.



Toa Maoni Yako:
0 comments: