Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Kitabu cha maombolezo ya Kifo cha aliyewahi kuwa mtangazaji wa Redio Tanzania, ITV na Redio One na Redio Aboud, marehemu Julius Nyaisanga, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita huko mjini Morogoro kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu. Marehemu Nyaisanya ameagwa leo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni na anasafirishwa leo hii kuelekea Tarime kwa ajili ya maziko. Picha Zote na Ofisi ya Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa mtangazaji wa Redio Tanzania, ITV na Redio One na Redio Aboud, marehemu Julius Nyaisanga, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita huko mjini Morogoro kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu. Marehemu Nyaisanya ameagwa leo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni na anasafirishwa leo hii kuelekea Tarime kwa ajili ya maziko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mfiwa Leah Nyaisanga, ambaye ni mke wa marehemu wa aliyewahi kuwa mtangazaji wa Redio Tanzania, ITV na Redio One na Redio Aboud, marehemu Julius Nyaisanga, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita huko mjini Morogoro kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu. Marehemu Nyaisanya ameagwa leo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni na anasafirishwa leo hii kuelekea Tarime kwa ajili ya maziko.
Leah Nyaisanga, ambaye ni mke wa marehemu wa aliyewahi kuwa mtangazaji wa Redio Tanzania, ITV na Redio One na Redio Aboud, marehemu Julius Nyaisanga, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu mumewe, aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita huko mjini Morogoro kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu, wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni na anasafirishwa leo hii kuelekea Tarime kwa ajili ya maziko.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, wakati wa shughuli hiyo Viwanja vya Leaders.
Sehemu ya Wanakamati wa Kamati ya maziko....
Sehemu ya waombolezaji waliojitokeza kumuaga marehemu Nyaisanga, katika Viwanja vya Leaders Club.
Kibanda, akizungumza machache........
Dkt. Reginald Mengi, akizungumza machache....
Sehemu ya waombolezaji waliojitokeza kumuaga marehemu Nyaisanga, katika Viwanja vya Leaders Club.
Freeman Mbowe, akizungumza machache.....
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akizungumza kutoka salam za rambirambi kwa wafiwa.
Mungu awafariji familia ya nyausanga. BWANA alitoa na yeye ametwaa. Jina lake libarikiwe. Amen
ReplyDelete