Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera, Jamal Malinzi amechaguliwa kuwa Rais Mpya wa shirikisho la soka nchini, TFF

Malinzi ameshinda uchaguzi huo wa leo uliokuwa ukifanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa NSSF, Water Front jijini Dar es Salaam kwa kupata asilimia 78 ya kura na kumbwaga mpinzani wake Athuman Nyamlani. Malinzi atachukua nafasi ya Leodegar Tenga aliyekuwa Rais wa TFF tangu mwaka 2005.

Kati ya 1999 na 2005, Malinzi alishika nyadhifa mbalimbali Yanga zikiwemo seneta, mkurugenzi wa kuchaguliwa, kaimu katibu mtendaji na katibu mkuu. Amekuwa mwenyekiti wa mashindano ya mpira wa miguu mkoa wa Pwani (2009 – 2011) na mjumbe wa Baraza la Michezo la Mkoa wa Dar es Salaam (2009-2012).

Toka 2011 hadi sasa ni mjumbe kwenye Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Miguu wilaya ya Misenyi, pia mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Kagera.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: