Pichani ni Mwandishi Ufo Saro akiwa na Rais Jakaya Kikwete. (Picha na Maktaba).

MWANDISHI wa ITV na Radio One, Ufo Saro amepigwa risasi tano maeneo mbali mbali ya mwili wake ikiwemo tumboni, Mbavuni na mguuni na kupelekea kumjeruhiwa vibaya, huku mama yake mzazi aitwaye Anastazia Saro kufariki baada ya kupigwa risasi chini ya maziwa katika tukio hilo.

Habari mpyaa za awali iliyofikia dawati letu la habari zinasema kuwa tukio hilo limewahusisha watu wanne ambao ni mwandishi huyo pamoja na mama yake na (mtoto ambaye alifanikiwa kukimbia eneo la tukio) ambao wamefanyiwa kitendo hicho na Mushi anayedaiwa kuwa ni mpenzi wa Ufo Saro, ambaye inadaiwa alikuwa nao katika mazungumzo nyumbani kwao Kibamba jijini la Dar es Salaam ndipo kijana huyo akadaiwa kuwafyatulia risasi na kisha na yeye kujifyatulia risasi ya kidevu kufa hapo hapo.
 
Baada ya tukio hilo mwandishi Ufo Saro ambaye hali yake ni mbaya alikimbizwa hospitali ya Tumbi Kibaha ila kwa sasa amehamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi na kuondolewa risasi zilizomo mwilini mwake.

Inavyosemekana Mushi ni mfanyakazi wa Shirika la UN.

Endelea kusoma Kajunason Blog uzidi kupata zinazoendelea.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

3 comments:

  1. Pole sana dada ufoo Mungu atakusaidia utapona

    ReplyDelete
  2. Hiyo ni hatari sana ila heri nusu shari kuliko shari kamili,nakuombea upone haraka Dada Ufoo

    ReplyDelete
  3. Hiyo ni hatari sana ila heri nusu shari kuliko shari kamili,nakuombea upone haraka Dada Ufoo

    ReplyDelete